Waziri
wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akikagua ghala la kuhifadhia mbolea
la Stamco katika eneo la Vwawa wilayani Mbozi wakati akiwa katika ziara
ya kikazi mkoani Songwe tarehe 22 Disemba 2019. (Picha Na Mathias Canal,
Wizara ya Kilimo)
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akikagua skimu ya Umwagiliaji ya Mbulu iliyopo katika kata ya Mahenje wilayani Mbozi wakati akiwa katika ziara ya kikazi mkoani Songwe tarehe 22 Disemba 2019.
Waziri
wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akikagua ghala la kuhifadhia mbolea
la Stamco katika eneo la Vwawa wilayani Mbozi wakati akiwa katika ziara
ya kikazi mkoani Songwe tarehe 22 Disemba 2019.
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akikagua skimu ya Umwagiliaji ya Mbulu iliyopo katika kata ya Mahenje wilayani Mbozi wakati akiwa katika ziara ya kikazi mkoani Songwe tarehe 22 Disemba 2019.
********************************
Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Songwe
Serikali imeeleza kuwa imekusudia
kuanzisha juhudi wezeshi kuhakikisha kuwa mbegu bora
za kilimo
zinazalishwa nchini ili kuondokana na wimbi la uagizaji wa mbegu nje ya
nchi.
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga
(Mb) ameyasema hayo tarehe 22 Disemba 2019 mara baada ya kutembelea
kampuni ya Namburi inayojihusisha na uzalishaji wa mbegu za vizazi za
mahindi, mtama na mpunga iliyopo katika eneo la Vwawa wilayani Mbozi
wakati akiwa katika ziara ya kikazi mkoani Songwe.
Amesema kuwa Tanzania ina uhitaji wa
mbegu kiasi cha Tani 186,000 za mazao mbalimbali huku uzalishaji wa
ndani ikiwa ni pamoja na uagizaji wa mbegu nje ya nchi ukiwa bado mdogo
kwani haujafika hata Tani 50,000.
Amesema kuwa Tanzania ina maeneo
makubwa na bora kwa uzalishaji hivyo ni lazima kuzalisha mbegu za
kutosha nchini na kuachana na utegemezi wa mbegu kutoka nje ya nchi.
Waziri Hasunga ametoa rai kwa
wananchi kuhakikisha kuwa wananunua mbegu bora kwa ajili ya kukabiliana
na msimu wa kilimo na kuachana na matumizi ya mazao yao ya misimu
iliyopita waliyoyahifadhi kama mbegu.
Katika ziara hiyo waziri Hasunga
amezungumza na wananchi wa kijiji cha Mbulu kilichopo katika kata ya
Mahenje wilayani Mbozi mara baada ya kukagua skimu ya umwagiliaji ya
Mbulu amesema kuwa serikali imedhamiria kuimarisha skimu za umwagiliaji
nchini ili kuondokana na kilimo cha kutegemea mvua.
Mhe Hasunga amesema kuwa kilimo cha
kutegemea mvua ni hatari kwani hakina uhakika wa upatikanaji wa chakula
cha kutosha kutokana na changamoto mbalimbali zinazojitokeza za
kukosekana kwa mvua kwa sababu ya mabadiliko ya tabia nchi.
Amewaagiza maafisa ugani kuzuru
katika maeneo ya wakulima ili kutoa elimu sahihi za kilimo, matumizi
sahihi ya viuatilifu pamoja na matumizi sahihi ya zana za kilimo.
Ameitaja Programu ya kuendeleza
kilimo awamu ya pili-ASDP II yenye jukumu la kuimarisha masoko na
kuongeza thamani kuwa ni lazima wakulima watumia njia bora za kilimo
ikiwa ni pamoja na kupata elimu bora na sahihi kwa wakulima.
Waziri Hasunga amesema kuwa katika
Programu hiyo ya kuendeleza kilimo awamu ya pili moja ya mambo msingi ni
matumizi bora ya maji na ardhi, hivyo sekta ya kilimo ni muhimili wa
matumizi bora ya maji kupitia skimu za umwagiliaji.
No comments :
Post a Comment