Saturday, November 30, 2019

WAHITIMU ADEM WAASWA KUTUMIA ELIMU WALIYOIPATA KUSAIDIA JAMII



Naibu Katibu Mkuu,OR TAMISEMI (Elimu), Mh.Gerald Mweli akisoma hotuba yake katika mahafali ya ishirini na saba ya ADEM kwa wahitimu wa stashahada za Uongozi na Usimamizi wa Elimu -DEMA,Ukaguzi wa shule-DSI na astashahada ya Uongozi na usimamizi wa Elimu-CELMA yaliyofanyika ADEM-Bagamoyo Mkoa wa Pwani.
Wahitimu wa Chuo cha ADEM Bagamoyo, Mwanza na Mbeya wakiwa katika Mahafali yao yaliyofanyika leo katika Chuo cha ADEM Bagamoyo Mkoani Pwani.
Naibu Katibu Mkuu,OR TAMISEMI (Elimu), Mh.Gerald Mweli akizindua machapisho ya Wakala ADEM na kuwakabidhi baadhi ya wadau mbalimbali wa elimu nchini, katika mahafali ya ishirini na saba ya ADEM kwa wahitimu wa stashahada za Uongozi na Usimamizi wa Elimu -DEMA,Ukaguzi wa shule-DSI na astashahada ya Uongozi na usimamizi wa Elimu-CELMA yaliyofanyika ADEM-Bagamoyo Mkoa wa Pwani.
Mtendaji Mkuu ADEM, Dkt.Dkt.SIston Mgullah akisoma hotuba yake mbele ya wahitimu, katika mahafali ya ishirini na saba ya ADEM kwa wahitimu wa stashahada za Uongozi na Usimamizi wa Elimu-DEMA,Ukaguzi wa shule-DSI na astashahada ya Uongozi na usimamizi wa Elimu-CELMA yaliyofanyika ADEM-Bagamoyo Mkoa wa Pwani.
**************************************
NA EMMANUEL MBATILO
Serikali imewataka wahitimu wa chuo cha ADEM nchini wanaporudi shuleni waweze kusimamia utekelezaji wa Sera ya Elimu na Mafunzo ya 2014, Sheria, Kanuni na Taratibu za Elimu ili kupunguza migogoro shuleni na kudhibiti
nidhamu za wanafunzi.
Ameyasema hayo leo Naibu Katibu Mkuu,OR TAMISEMI (Elimu), Mh.Gerald Mweli katika
mahafali ya ishirini na saba ya ADEM kwa wahitimu wa stashahada za Uongozi na Usimamizi wa Elimu _DEMA,Ukaguzi wa shule-DSI na astashahada ya Uongozi na usimamizi wa Elimu-CELMA yaliyofanyika ADEM-Bagamoyo Mkoa wa Pwani.
Akizungumza katika mahafali hayo Mh.Mweli amewataka wahitimu kusimamia
utekelezaji wa Mtaala kwa ufanisi mkubwa, kutoa takwimu sahihi
za shule, kupanga mipango ya maendeleo ya shule
inayotekelezeka, kusimamia fedha na rasilimali zingine za shule,
kusimamia ustawi wa walimu na wanafunzi, kushirikisha jamii na
wadau wa Elimu katika shughuli za maendeleo ya shule pamoja
na kufanya ufuatiliaji na tathmini wa shughuli zinazotekelezwa
shuleni.
“Ninawataka mkaoneshe kwa vitendo elimu mliyoipata
katika kutumikia nafasi mbalimbali mtakazopangiwa na waajiri
wenu. Ninashawishika kusema kwamba, ninyi ndiyo mabalozi na
kioo cha chuo hiki katika kutoa mfano wa uongozi na utawala bora, uchapaji kazi, uzalendo pamoja na uadilifu katika kulitumikia
Taifa letu”. Amesema Mh.Mweli.
Aidha, Mh.Mweli amesema kuwa kwa mwaka 2018/2019, ADEM
iliendesha mafunzo ya Mtaala mpya na uimarishaji wa stadi za
Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK) kwa jumla wa walimu
1,598. Mafunzo haya yaliendeshwa kwa Mikoa iliyokuwa na udahili mkubwa kwa darasa la Kwanza.
“Mafunzo mengine yalitolewa kwa Maafisa Elimu Kata wapatao 3,910 kuhusu
uanzishaji na usimamizi wa shule/ madarasa ya Elimu ya Awali
pamoja na Wakuu wa Shule za Sekondari wapatao 349″.Amesema.
Pamoja na hayo, Mh.Mweli amesema kuwa Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli imedhamiria kuongeza wigo wa kupata elimu bora nchini.
“Hatua kadhaa zimeshachukuliwa na utekelezaji wake
unaonekana. Baadhi ya hatua hizo ni kutoa elimu bila ada kwa
lengo la kuongeza fursa ya watoto wengi kupata ElimuMsingi,
kuboresha Mitaala kwa lengo la kujenga umahiri unaotakiwa
katika kila ngazi ya Elimu, kutoa mafunzo ya kuwajengea uwezo walimu na kukarabati Vyuo vya Ualimu na shule kongwe za Sekondari”. Amesema Mh.Mweli.
Kwa upande wake Mtendaji Mkuu wa Chuo cha ADEM Dkt.Siston Mgullah amesema kuwa kiwango cha ufaulu kwa Wahitimu wa kozi ya Uongozi na Usimamizi wa Elimu (DEMA) unaonesha kuwa wahitimu 99(10.74%) wamepata Daraja la Kwanza (First Class), wahitimu 571(61.99%) wamepata Daraja la Pili la Juu (Upper Second Class), Wahitimu 248(26.92%) wamepata Daraja la Pili la
Kawaida (Lower Second Class) na wahitimu 3(0.32%) wamepata Daraja la
Kawaida(Pass).
Aidha Dkt.Mghullah amesema kuwa Kiwango cha ufaulu kwa upande wa Wahitimu wa Kozi ya Stashahada ya Ukaguzi wa Shule (DSI) unaonesha kuwa wahitimu 69(25.74%) wamepata Daraja la Kwanza (First Class), wahitimu 163(60.82%) wamepata Daraja la Pili la Juu (Upper Second Class), Wahitimu 35(13.05%) wamepata Daraja la Pili la Kawaida (Lower Second Class) na Mhitimu 1(0.37%) amepata Daraja la Kawaida (Pass).
Amesema kuwa Kiwango cha ufaulu kwa upande wa Wahitimu wa Kozi ya Astashahada ya Uongozi na Usimamizi wa Elimu (CELMA) unaonesha kuwa mhitimu mmoja(33.3%) amepata Daraja la Pili na wahitimu 2(66.7%) wamepata Daraja la Kawaida.
Dkt.Mgullah amemaliza kwa kusema kuwa  mategemeo yao kuwa wahitimu wa kozi ya Uongozi na Usimamizi wa elimu kwa ngazi za Astashahada na Stshahada wataweza kuongoza vizuri shule, kupanga mipango inayotekelezeka, kusimamia utekelezaji wa mtaala pamoja na upimaji wa maendeleo ya wanafunzi kwa umahiri.
“Katika kuboresha utendaji kwa wahitimu wetu, ADEM imeongeza baadhi ya
masomo ya kufundishia kwa walimu wanaosoma kozi za DEMA na DSI
ambayo ni: TEHAMA (ICT), Hisabati, Kiswahili na Stadi zake, Historia,
Jiografia na Kiingereza. Hii ni hatua muhimu katika mageuzi ya kifikra kwa
wahitimu wetu. Tunaamini kuwa kiongozi mzuri ni yule anayekuwa na
uelewa mpana wa kazi yake. Hivyo, kujumuisha masomo ya kufundishia
katika mtaala kutamsaidia mhitimu wetu kufanya ufuatiliaji na tathmini ya
shughuli za ufundishaji kwa weledi mkubwa zaidi”. Amesema

No comments :

Post a Comment