Waziri wa Elimu, Sayansi na
Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako akizungumza wakati wa uzinduzi wa
Ujenzi wa Chuo cha mafunzo ya Ufundi Stadi na Huduma cha Mkoa wa Kagera
mkoani Kagera.
Balozi wa China nchini Tanzania
WANG Ke akizungumza wakati wa uzinduzi wa Ujenzi wa Chuo cha Mafunzo ya
Ufundi Stadi na Huduma Cha Mkoa wa Kagera.
Baadhi ya Wanafunzi wa Chuo cha
ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi waliohudhuria uzinduzi wa ujenzi wa
chuo cha VETA cha Mkoa wa Kagera wakifuatilia hotuba ya waziri wa Elimu,
Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako.
Waziri wa Elimu, Sayansi na
Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako akizindua kuanza kwa ujenzi wa Chuo
cha Mafunzo ya Ufundi Stadi na Huduma cha mkoa wa Kagera, mkoani Kagera.
Waziri wa Elimu, Sayansi na
Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako akishikana mkono na Balozi wa China
nchini Tanzania mara baada ya uzinduzi wa ujenzi wa Chuo cha VETA cha
mkoa wa Kagera.
Waziri wa Elimu, Sayansi na
Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako, Balozi wa China nchini Tanzania WANG
Ke pamoja na viongozi wengine wa mkoa wa Kagera wakiweka udongo kwenye
mti ikiwa ni sehemu ya uzinduzi wa ujenzi wa Chuo cha Mafunzo ya Ufundi
Stadi na Huduma cha Mkoa wa Kagera.
Waziri wa Elimu, Sayansi na
Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako akiteta jambo na Mkuu wa Mkoa wa
Kagera Brigedia Generali Marco Gaguti wakati wa uzinduzi wa ujenzi wa
Chuo cha VETA cha mkoa wa Kagera.
Waziri wa Elimu, Sayansi na
Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako akiwasili katika hafla ya uzinduzi wa
ujenzi wa Chuo cha VETA cha mkoa wa Kagera.
…………………..
Na.Alex Sonna,Dodoma
Waziri wa Elimu, Sayansi na
Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako amezindua ujenzi wa Chuo cha Ufundi
Stadi na Huduma cha Mkoa wa Kagera na kusema kuwa ujenzi wa chuo hicho
ni muendelezo wa jitihada za Serikali ya Awamu ya Tano kuhakikisha
kunakuwa na Vyuo vya ufundi stadi vya Mikoa na Wilaya.
Akizindua ujenzi wa chuo hicho
mkoani Kagera Waziri Ndalichako amesema chuo hicho
kinajengwa na
Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China kutokana na uhusiano mzuri wa muda
mrefu tulio nao na kwamba pindi ujenzi utakapokamilika vijana wengi wa
kitanzania watapata fursa ya kusoma katika chuo hicho na kupata ujuzi
katika fani mbalimbali zitakazo fundishwa.
“Kama nilivyosema Tanzania na
China ni marafiki na rafiki yako anaangalia mahitaji yako, waswahili
husema akufaaye kwa dhiki ndio rafiki wa kweli. China imeona Tanzania
inajenga uchumi wa Viwanda ikiwa ni azma ya serikali ya awamu ya Tano
nao wakaamua watuunge mkono katika ujenzi wa Chuo cha Ufundi stadi ili
kuandaa vijana wenye ujuzi watakaofanya kazi katika viwanda.
“Nikuombe Balozi tufikishie
shukrani zetu za dhati kwa Rais wa Serikali ya Jamhuri ya watu wa China
kwa msaada huu mkubwa na wa kihistoria ,”aliongeza Waziri Ndalichako
Waziri Ndalichako amesema ujio wa
mradi huo utaongeza ajira kwa vijana wa kitanzania kwa kuwa wazawa 400
wataajiriwa katika mradi huo ikiwa ni pamoja na kupata ujuzi kulingana
na kazi watakazokuwa wakizitekeleza.
“Vijana watakaofanya kazi eneo la
mradi pamoja na kufanya kazi watapata na mafunzo, kwa hiyo ujuzi wao wa
kiufundi utaimarishwa kupitia kazi ambazo watakuwa wakifanya katika
mradi,”alisema waziri Ndalichako.
Katika hatua nyingine Waziri
Ndalichako ameitaka Mamlaka ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi VETA
kupitia upya fani zilizopangwa kutolewa katika chuo hicho ili ziendane
na Mazingira halisi ya kiuchumi kwa wakazi wa eneo hilo.
“Nimepitia fani ambazo zimeanishwa
kutolewa katika chuo hiki pindi kitakapokamilika, nikiangalia eneo
ambalo chuo kinajengwa ni eneo la ziwa na watu wa Kagera au wazazi wa
hapa ni wavuvi lakini sijaona kozi ya uvuvi sasa tunawaletea mambo ya
uchomeleaji, ufundi bomba, useremala, upakaji rangi kwenye bahari,
nilitegemea kuwe na fani ya uvuvi pia
tuweke fani zinazoendana na mazingira,” alisema Waziri Ndalichako
tuweke fani zinazoendana na mazingira,” alisema Waziri Ndalichako
Kwa upande wake Balozi wa China
nchini Tanzania Balozi WANG Ke amesema Rais wa Jamhuri wa Muungano wa
Tanzania amezingatia maboresho ya sekta ya elimu ikiwa ni pamoja na
kuwaongoza watanzania kuelekea dira ya maendeleo 2025 hivyo China iko
tayari kuchangia maendeleo katika sekta ya elimu ili kufikia malengo ya
elimu ambayo serikali ya tanzania imejiwekea.
Nae Mkuu wa mkoa wa Kagera
Brigedia Generali Marco Gaguti amewataka wanakagera hasa vijana
kushiriki vizuri katika kazi za ujenzi zitakazofanyika katika mradi huo
ili kupata ujuzi wa ufundi ambao utawasaidia kushirikia katika kazi za
ujenzi zitakazojitokeza katika Mkoa wa Kagera mara baada ya mradi
kukamilika.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya
Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi VETA Dkt. Pancras Bujulu amesema Chuo
hicho kinajengwa katika eneo lililotolewa na wananchi wa kijiji cha
Burugo wilayani Bukoba na lina ukubwa wa hekta 40. 5 sawa na hekari 100.
Dkt. Bujulu amesema Chuo hicho
pindi kitakapokamilika kitatoa fani za useremala, uchomeleaji, upakaji
rangi, ufundi bomba na kitachukua wanafunzi 800 wa kozi ndefu na 2000 wa
kozi fupi
Chuo cha Ufundi na Mafunzo ya
Ufundi Stadi cha Mkoa wa Kagera kinajengwa kwa msaada wa Serikali ya
Jamhuri ya Watu wa China kwa gharama za fedha za kitanzania sh bilioni
19.4 ambapo ujenzi wake utachukua miezi 18
Gharama hizo zinajumuisha usanifu, upembuzi yakinifu na ujenzi mpaka ukamilike.
No comments :
Post a Comment