Friday, November 1, 2019

Vodacom yazindua Smart Kitochi, Simu janja ya kwanza Tanzania inayopatikana kwa bei rahisi kutoka KaiOS

Mkuu wa Kitengo cha mauzo na usambazaji wa Vodacom Tanzania Plc,George Lugata (kushoto) akitambulisha simu mpya ya kitochi yenye 4G na zana za simu janja inayofahamika kwa jina la Smart Kitochi kwa waandishi wa habari jana, inayotumia KaiOS, mfumo ambao unaongoza duniani katika teknolojia ya simu janja, ni ya kwanza kupatikana katika soko nchini Tanzania kwa kiasi cha Tsh 48,000 ikiwa na kifurushi cha GB 4, dakika 100 za maongezi na SMS 500 kwa kila mwezi ndani ya miezi sita ya kwanza.Wengine ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano  na uhusiano cha kampuni hiyo Jacquiline Materu na balozi wa Smart Kitochi, Sylvester Mujuni maarufu kama Mpoki.

Mteja wa kwanza kununua simu mpya ya kitochi yenye 4G na zana za simu janja Smart Kitochi, Lydia Mtei mkazi wa Mbezi Beach akipata maelezo kutoka kwa Mkuu wa Kitengo cha mauzo na usambazaji wa Vodacom Tanzania Plc,George Lugata mara baada ya kuzindua simu hiyo kwenye duka la Vodashop mlimani city jana ambapo itapatikana katika maduka yote ya Vodacom nchini. Wengine ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na uhusiano cha kampuni hiyo Jacquiline Materu na balozi wa Smart Kitochi, Sylvester Mujuni maarufu kama Mpoki.

Balozi wa Smart Kitochi, Sylvester Mujuni maarufu kama Mpoki akielezea zana zilizomo ndani ya  Smart Kitochi mbele ya waandishi wa habari jana, Vodacom ni kampuni ya kwanza nchini kuleta simu ya kitochi yenye uwezo wa simu janja kwa kupata huduma za Apps muhimu kama vile WhatsApp, Google Assistant, Facebook, YouTube na nyingine nyingi.

Baadhi ya wateja waliojitokeza kununua simu za Smart Kitochi jana kwenye duka la Vodacom Mlimani city jijini Dar Es Salaam.
……………………………………………………

  • Simu inapatikana katika maduka yote ya Vodacom nchini
  • Wateja kupata data, muda wa maongezi na SMS bure kwa miezi 6 ya kwanza

Kampuni inayoongoza kwa teknolojia ya Mawasiliano Tanzania, Vodacom, leo inatangaza
uzinduzi wa simu mpya inayofahamika kwa jina la Smart Kitochi. Simu hii inatumia KaiOS, mfumo ambao unaoongoza duniani katika teknolojia ya simu janja.
Uzinduzi huu unaongeza hatua kubwa si kwa kampuni hizi mbili tu, bali hata kwa nchi. Ni simu janja ya kwanza kupatikana katika soko nchini Tanzania kwa kiasi cha Tsh 48,000 (Dola 20 za Marekani) ikiwa na kifurushi cha GB 4, dakika 100 za maongezi na SMS 500 kwa miezi sita ya kwanza.
Smart Kitochi inatumia apps muhimu kama vile WhatsApp, Google Assistant, Facebook, YouTube na nyingine nyingi zikiwapa fursa watanzania kujiunga na huduma ya inteneti. Ikiwa na sifa zote za simu janja kama vile kuwa na Wi-Fi, GPS, simu hii ina uwezo wa kutumia laini mbili zenye uwezo wa uhifadhi wa GB 4 + MB 512. Pia ina betri yenye nguvu ya mAh 1400 na kudumu saa sita. Ikiwa inazinduliwa leo hapa nchini, simu hii pia itaanza kupatikana katika nchi nyingine za Afrika hivi karibuni.
 “Tuna furaha kuwaleteeni simu hii mpya sokoni kwa ushirikiano na mshirika wetu KaiOS Technologies,” anasema  George Lugata, Mkuu wa Kitengo cha Mauzo wa Vodacom. “Pamoja na uwepo wa matumizi makubwa katika mtandao wa mawasiliano nchini, bado tunakumbana na changamoto za kidigitali kwa sababu ya uwepo mdogo wa matumizi ya simu janja, kwa kufanya hivyo tunawaletea Smart Kitochi kwa bei nafuu kwa kila mtu. 
KaiOS inatumia mfumo mwepesi kabisa ambao una sifa zote za simu janja ambazo ni pamoja na kuwa na uwezo wa kutosha wa uhifadhi. Pamoja na sifa hizo simu hiyo inatumia mifumo  ya 3G na 4G/LTE, Wi-Fi, GPS, pamoja na NFC. 
Simu ya KaiOS inakuja ikiwa na apps maarufu kama WhatsApp, Google Assistant, Facebook, YouTube, and Google Maps. Halikadhalika simu hii ina app ya KaiStore, ambayo ni kati ya apps zaidi ya 200 zinazotumiwa na watoa huduma mbalimbali wa mawasiliano duniani.
 KaiOS Technologies ni ya tatu kwa ukubwa duniani katika mfumo wa utoaji huduma za mawasiliano ya kidigitali, ikiwa na zaidi ya aina 100 za vifaa vinavyosambazwa katika Mabara ya Ulaya, Afrika, Asia na Marekani.
“Mgawanyiko wa matumizi ya mfumo wa kidigitali Afrika bado ni mpana. Tumejikita zaidi katika kutoa fursa pamoja na kuleta teknolojia mpya yenye utatuzi wa mambo mbambali na ndiyo maana tumeamua kufanya kazi na Vodacom. Smart Kitochi ni hatua moja muhimu katika kuuwaunganisha wale ambao walikuwa nyuma katika matumizi ya inteneti na rasilimali zote muhimu za mawasiliano nchini na kwingineko’” anasema Afisa Mtendaji Mkuu wa KaiOS Technologies, Sebastien Codeville.
 “Simu ya Smart Kitochi inapatikana katika maduka yote ya Vodashop nchini na katika vituo vyote vya huduma na mauzo ya bidhaa zetu nchini kote kwa bei ya punguzo ya Tsh 48,000. Niwaombe Watanzania na hasa wateja wetu kujitokeza kununua simu hii  ili waweze kufurahia huduma za Mtandao Supa na kufurahia apps kama vile Facebook, WhatsApp, YouTube, Instagram na nyingine nyingi zinazopatikana katika simu janja,” alihitimisha Lugata.
Mwisho
Kuhusu Vodacom:
Vodacom Tanzania PLC ni watoa huduma ya mawasiliano ya simu za mkononi wanaoongoza wenye mtandao wa data wenye kasi zaidi nchini. Tunatoa huduma za mawsiliano kwa zaidi ya wateja milioni 14. Kampuni ya Vodacom Tanzania pamoja na kampuni zake tanzu ni sehemu ya Kundi la makampuni ya Vodacom (Vodacom Group) iliyosajiliwa Afrika Kusini ambayo kwa upande mwingine inamilikiwa na kundi la makampuni la Vodacom Plc la Uingereza. Kampuni ya Vodacom imesajiliwa katika soko la hisa la Dar es salaam (DSE) kwa namba ISIN: TZ1886102715 Stock name: VODA.
Kampuni inayoongoza kwa teknolojia ya Mawasiliano Tanzania, Vodacom, leo inatangaza uzinduzi wa simu mpya inayofahamika kwa jina la Smart Kitochi. Simu hii inatumia KaiOS, mfumo ambao unaoongoza duniani katika teknolojia ya simu janja.

No comments :

Post a Comment