Mkuu
wa Kitengo cha mauzo na usambazaji wa Vodacom Tanzania Plc,George
Lugata (kushoto) akitambulisha simu mpya ya kitochi yenye 4G na zana za
simu janja inayofahamika kwa jina la Smart Kitochi kwa waandishi wa
habari jana, inayotumia KaiOS, mfumo ambao unaongoza duniani katika
teknolojia ya simu janja, ni ya kwanza kupatikana katika soko nchini
Tanzania kwa kiasi cha Tsh 48,000 ikiwa na kifurushi cha GB 4, dakika
100 za maongezi na SMS 500 kwa kila mwezi ndani ya miezi sita ya
kwanza.Wengine ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na uhusiano cha
kampuni hiyo Jacquiline Materu na balozi wa Smart Kitochi, Sylvester
Mujuni maarufu kama Mpoki.
Mteja
wa kwanza kununua simu mpya ya kitochi yenye 4G na zana za simu janja
Smart Kitochi, Lydia Mtei mkazi wa Mbezi Beach akipata maelezo kutoka
kwa Mkuu wa Kitengo cha mauzo na usambazaji wa Vodacom Tanzania
Plc,George Lugata mara baada ya kuzindua simu hiyo kwenye duka la
Vodashop mlimani city jana ambapo itapatikana katika maduka yote ya
Vodacom nchini. Wengine ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na uhusiano
cha kampuni hiyo Jacquiline Materu na balozi wa Smart Kitochi, Sylvester
Mujuni maarufu kama Mpoki.
Balozi
wa Smart Kitochi, Sylvester Mujuni maarufu kama Mpoki akielezea zana
zilizomo ndani ya Smart Kitochi mbele ya waandishi wa habari jana,
Vodacom ni kampuni ya kwanza nchini kuleta simu ya kitochi yenye uwezo
wa simu janja kwa kupata huduma za Apps muhimu kama vile WhatsApp,
Google Assistant, Facebook, YouTube na nyingine nyingi.
Baadhi ya wateja waliojitokeza kununua simu za Smart Kitochi jana kwenye duka la Vodacom Mlimani city jijini Dar Es Salaam.
……………………………………………………
- Simu inapatikana katika maduka yote ya Vodacom nchini
- Wateja kupata data, muda wa maongezi na SMS bure kwa miezi 6 ya kwanza
Kampuni inayoongoza kwa
teknolojia ya Mawasiliano Tanzania, Vodacom, leo inatangaza
uzinduzi wa
simu mpya inayofahamika kwa jina la Smart Kitochi. Simu hii inatumia
KaiOS, mfumo ambao unaoongoza duniani katika teknolojia ya simu janja.
Uzinduzi huu unaongeza hatua
kubwa si kwa kampuni hizi mbili tu, bali hata kwa nchi. Ni simu janja ya
kwanza kupatikana katika soko nchini Tanzania kwa kiasi cha Tsh 48,000
(Dola 20 za Marekani) ikiwa na kifurushi cha GB 4, dakika 100 za
maongezi na SMS 500 kwa miezi sita ya kwanza.
Smart Kitochi inatumia apps
muhimu kama vile WhatsApp, Google Assistant, Facebook, YouTube na
nyingine nyingi zikiwapa fursa watanzania kujiunga na huduma ya
inteneti. Ikiwa na sifa zote za simu janja kama vile kuwa na Wi-Fi, GPS,
simu hii ina uwezo wa kutumia laini mbili zenye uwezo wa uhifadhi wa GB
4 + MB 512. Pia ina betri yenye nguvu ya mAh 1400 na kudumu saa sita.
Ikiwa inazinduliwa leo hapa nchini, simu hii pia itaanza kupatikana
katika nchi nyingine za Afrika hivi karibuni.
“Tuna furaha kuwaleteeni simu
hii mpya sokoni kwa ushirikiano na mshirika wetu KaiOS Technologies,”
anasema George Lugata, Mkuu wa Kitengo cha Mauzo wa Vodacom. “Pamoja na
uwepo wa matumizi makubwa katika mtandao wa mawasiliano nchini, bado
tunakumbana na changamoto za kidigitali kwa sababu ya uwepo mdogo wa
matumizi ya simu janja, kwa kufanya hivyo tunawaletea Smart Kitochi kwa
bei nafuu kwa kila mtu.
KaiOS inatumia mfumo mwepesi
kabisa ambao una sifa zote za simu janja ambazo ni pamoja na kuwa na
uwezo wa kutosha wa uhifadhi. Pamoja na sifa hizo simu hiyo inatumia
mifumo ya 3G na 4G/LTE, Wi-Fi, GPS, pamoja na NFC.
Simu ya KaiOS inakuja ikiwa na
apps maarufu kama WhatsApp, Google Assistant, Facebook, YouTube, and
Google Maps. Halikadhalika simu hii ina app ya KaiStore, ambayo ni kati
ya apps zaidi ya 200 zinazotumiwa na watoa huduma mbalimbali wa
mawasiliano duniani.
KaiOS Technologies ni ya tatu
kwa ukubwa duniani katika mfumo wa utoaji huduma za mawasiliano ya
kidigitali, ikiwa na zaidi ya aina 100 za vifaa vinavyosambazwa katika
Mabara ya Ulaya, Afrika, Asia na Marekani.
“Mgawanyiko wa matumizi ya mfumo
wa kidigitali Afrika bado ni mpana. Tumejikita zaidi katika kutoa fursa
pamoja na kuleta teknolojia mpya yenye utatuzi wa mambo mbambali na
ndiyo maana tumeamua kufanya kazi na Vodacom. Smart Kitochi ni hatua
moja muhimu katika kuuwaunganisha wale ambao walikuwa nyuma katika
matumizi ya inteneti na rasilimali zote muhimu za mawasiliano nchini na
kwingineko’” anasema Afisa Mtendaji Mkuu wa KaiOS Technologies,
Sebastien Codeville.
“Simu ya Smart Kitochi
inapatikana katika maduka yote ya Vodashop nchini na katika vituo vyote
vya huduma na mauzo ya bidhaa zetu nchini kote kwa bei ya punguzo ya Tsh
48,000. Niwaombe Watanzania na hasa wateja wetu kujitokeza kununua simu
hii ili waweze kufurahia huduma za Mtandao Supa na kufurahia apps kama
vile Facebook, WhatsApp, YouTube, Instagram na nyingine nyingi
zinazopatikana katika simu janja,” alihitimisha Lugata.
Mwisho
Kuhusu Vodacom:
Vodacom Tanzania PLC ni watoa
huduma ya mawasiliano ya simu za mkononi wanaoongoza wenye mtandao wa
data wenye kasi zaidi nchini. Tunatoa huduma za mawsiliano kwa zaidi ya
wateja milioni 14. Kampuni ya Vodacom Tanzania pamoja na kampuni zake
tanzu ni sehemu ya Kundi la makampuni ya Vodacom (Vodacom Group)
iliyosajiliwa Afrika Kusini ambayo kwa upande mwingine inamilikiwa na
kundi la makampuni la Vodacom Plc la Uingereza. Kampuni ya Vodacom
imesajiliwa katika soko la hisa la Dar es salaam (DSE) kwa namba ISIN:
TZ1886102715 Stock name: VODA.
Kampuni inayoongoza kwa
teknolojia ya Mawasiliano Tanzania, Vodacom, leo inatangaza uzinduzi wa

No comments:
Post a Comment