Spika wa Bunge la Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai akiongea viongozi wa dini (hawapo
pichani) wakati wa mkutano wa viongozi wa dini wa Taifa na wa kanda ya
ziwa ambapo viongozi hao walitia saini maazimio ya mapambano dhidi ya
kifua kikuu jijini Mwanza
Baadhi ya viongozi wa dini wakimsikiliza mgeni rasmi wakati wa mkutano huo
Waziri wa Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akibadilishana mawazo na
Naibu Waziri wa OR-TAMISEMI Josephat Kandege kwenye mkutano wa viongozi
wa dini katika vita dhidi ya Kifua Kikuu
Viongozi mbalimbali wa dini wakifuatilia mkutano huo ambao umefanyika kwenye ukumbi wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mwanza
Waziri wa Afya Ummy Mwalimu
akiongea wakati wa mkutano wa viongozi wa dini ambapo alisema wanayo
imani na viongozi wa dini kwani wanawafikia wananchi wengi
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongella akiongea na viongozi hao
Viongozi wa dini wakisaini
maazimio ya kushiriki mapambano ya kutokomeza kifua kikuu.Mkutano huo
umeandaliwa na Bunge kupitia mtandao wa wabunge wa kupambana na kifua
kikuu
……………..
Na. Catherine Sungura, Mwanza
Serikali ya Tanzania inatenga
mabilioni mengi katika kushughulikia masuala ya afya nchini hususani
kwenye upande wa tiba ambapo gharama za matibabu zinakuwa kubwa sana.
Hayo yamesemwa leo na Spika wa
Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai wakati kusaini
tamko la maazimio ya viongozi wa dini lililobeba ajenda ya mapambano
dhidi ya ugonjwa wa Kifua kikuu (TB) ,makazi na lishe bora nchini
jijini hapa
“Wananchi wanadhani kuwa wizara
ya afya inasimamia tu tiba, hapana tusisahau kinga ni muhimu sana dhidi
ya magonjwa nchini, tutakaposimamia kinga serikali itakua inaokoa
gharama kubwa kwenye matibabu na pia kupunguza mzigo mkubwa wa
kugharamia matibabu kama nchi”Alisisitiza Mhe. Ndugai
Aidha, amewashuru viongozi hao
wa dini kwa ahadi pamoja na kusaini azimio la kusimamia na kusemea kwa
waumini wao suala zima la TB hivyo anayo Imani watalibeba na
kulitekeleza na kuwafanya wananchi wengi kupata uelewa juu ya ugonjwa
huo na kujitokeza mapema kwenda kupima afya zao na hivyo kuanza dawa
na kutoambukiza watu wengine.
Awali akiongea na viongozi hao
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy
Mwalimu amesema kuwa Wizara yake inaendelea kubuni mikakati ya
kutokomeza Tb nchini kama mikakati Madhubuti yaliyowekwa kwa mara ya
kwanza na baraza kuu la umoja wa mataifa lililokutana Septemba mwaka
2018 na kuweka maazimio na malengo ya kuongeza kasi ya kutokomeza TB
ifikapo mwaka 2030.
“Maambukizi mapya ya Tb nchini
yamepungua kwa asilimia 18 kulinganisha na hali ya mwaka 2015 na hivyo
kufanya Tanzania kuwa miongoni mwa nchi saba Duniani ambazo zipo
katika mwelekeo sahihi wa kufikia malengo ya mpango mkakati wa Shirika
la Afya Duniani (WHO) ya kutokomeza TB kwa hatua ya kwanza ya mwaka
2020.
Aidha, Waziri Ummy amesema kuwa
vifo vitokanavyo na Tb peke yake vimepungua kutoka 30,000 mwaka 2015
hadi 22,000 mwaka 2018 na hii ni sawa na punguzo la asilimia 27,“licha
ya mafanikio, nchi bado ina vifo vingi vinavyosababishwa na Tb ambapo
kwa sasa takribani watu sitini hufariki kila siku hapa nchini”,
alisema .
Hata hivyo Waziri huyo wa afya
amesema kuwa hadi kufikia mwaka huu serikali ina vituo 103 vinavyotoa
huduma za wagonjwa wenye Tb sugu ukilinganishwa na kituo kimoja mwaka
2015 pamoja na uboreshaji wa mifumo ya uchunguzi na ugunduzi wa TB
kwenye vituo vya huduma za afya,upanuzi wa matumizi ya hadumini za
kisasa za LED na kuongezeka kwa mashine za kisasa zinazopima vimelea vya
TB kwa njia ya vina saba za GenXpert zipatazo 238 ambazo kwa sasa
zinapatikana kwenye mikoa yote nchini.
No comments :
Post a Comment