Friday, November 29, 2019

BENKI KUU YAKANA KUJIHUSISHA NA FEDHA ZA KIMTANDAO




Benki Kuu ya Tanzania imeonya kuacha mara moja kuihusisha na shughuli za fedha za kimtandao 
(cyptocurrencies) kunakofanya na baadhi ya watu wanaojihusisha na biashara hiyo
haramu. Watu hao, 
ambao wanaleta usumbufu hapa nchini na nje, wamekuwa wakidai kwamba shughuli zao zinaungwa 
mkono na Benki Kuu ya Tanzania jambo ambalo halina ukweli wowote. 
Ikumbukwe kwamba mnamo Novemba 12, 2019, Benki Kuu ya Tanzania ilitoa taarifa kwa umma 
ikiwataka wananchi kujiepusha uuzaji, uhamasishaji na matumizi ya fedha za kimtandao kwani kufanya 
hivyo ni kinyume cha kanuni za udhibiti wa fedha za kigeni. 
Aidha, taarifa hiyo ilieleza kwamba fedha halakwa ajili ya kufanya malipo hapa Tanzania ni Shilingi ya 
Tanzania ambayo inatolewa na Benki Kuu. Benki Kuu ni taasisi pekee hapa nchini yenye mamlaka ya 
kuchapisha noti na kutengeneza sarafu na kuamua fedha halali kwa ajili ya matumizi hapa nchini, kama 
ilivyoainishwa kwenye Vifungu vya 26 na 27 vya Sheria ya Benki Kuu ya Tanzania ya mwaka 2006. 
Pia, fedha zote za kigeni zinazokubalika zinauzwa na kununuliwa na taasisi zilizosajiliwa nchini kwa 
mujibu wa Sheria ya Fedha za Kigeni ya 1992 na Kanuni zake. Kwa hivi sasa mfumo wa usimamizi na 
udhibiti wa fedha za kigeni nchini Tanzania hautambui biashara au matumizi ya fedha za kimtandao. 
Benki Kuu ya Tanzania inarudia kuwatahadharisha wananchi kutojihusisha na fedha za kimtandao na 
kwamba kufanya hivyo ni kinyume cha sheria. Imetolewa na: 
Idara ya Uhusiano wa Umma na Itifaki botcommunications@bot.go.tz 

No comments :

Post a Comment