CAG aliyemaliza Muda wake Prof. Mussa Assad Akimkaribisha CAG mpya,
Bw. Charles Kichere Kabla ya Makabidhiano ya Ofisi ya Mkaaguzi Mkuu na Mdhibiti wa Hesabu za Serikali(CAG), yaliyofanyika Jijini Dar es Salaam.
Bw. Charles Kichere Kabla ya Makabidhiano ya Ofisi ya Mkaaguzi Mkuu na Mdhibiti wa Hesabu za Serikali(CAG), yaliyofanyika Jijini Dar es Salaam.
AG aliyemaliza Muda wake Prof. Mussa Assad akieleza jambo kwa
Waandishi wa Habari(Hawapo pichani) kuhusu makabidhiano ya Ofisi ya Mkaaguzi Mkuu na Mdhibiti wa Hesabu za Serikali(CAG), yaliyofanyika Jijini Dar es Salaam, kushoto ni CAG mpya, Bw. Charles Kichere.
Waandishi wa Habari(Hawapo pichani) kuhusu makabidhiano ya Ofisi ya Mkaaguzi Mkuu na Mdhibiti wa Hesabu za Serikali(CAG), yaliyofanyika Jijini Dar es Salaam, kushoto ni CAG mpya, Bw. Charles Kichere.

CAG aliyemaliza Muda wake Prof. Mussa Assad akimkabidhi nyaraka za Ofisi
CAG mpyaBw. Charles Kichele katika Makabidhiano ya Ofisi ya Mkaaguzi Mkuu na Mdhibiti wa Hesabu za Serikali(CAG), yaliyofanyika Jijini Dar es Salaam.
CAG mpyaBw. Charles Kichele katika Makabidhiano ya Ofisi ya Mkaaguzi Mkuu na Mdhibiti wa Hesabu za Serikali(CAG), yaliyofanyika Jijini Dar es Salaam.
***************************************
Na.Mwandishi Wetu-MAELEZO
05-11-2019
Mdhibiti na
Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) mpya, Bw. Charles Kichere
amesema kuwa ataendelea kutekeleza majukumu ambayo yameachwa na CAG
aliyemaliza
muda wake Prof.Mussa Assad kwani Ofisi hiyo ni muhimu kwa
maendeleo ya watanzania.
Akizungumza
katika makabidhiano Kichere alisema kuwa Ofisi ya CAG ni nguzo muhimu
kwa watanzani kwani ndiyo ofisi inayolinda na kuangalia matumizi sahihi
ya kodi yao wanayolipa kila siku.
“Tutaendelea
kuifanyakazi ambayo imefanywa na Prof.Assad na timu yake, nitahakikisha
kushirikiana na wafanyakazi wa Ofisi hii kuifanya kazi hii ya kulinda
mapato ya kodi ya watanzania”, Alisema Kichere.
Kichere
alisema kuwa katika kutekeleza majukumu hayo mapya atahakikisha kuwa
atalinda Kodi ya watanzania wakulima, wafugaji, wavuvi, wafanyabiashara
na wafanyakazi ili fedha inayopataikana kwenye kodi iweze kuwanufaisha
wote.
Aliwahakikishia
watanzania kuwa hakuna kodi inayotolewa na watanzania ambayo itapotea
kwa hiyo ataangalia na kuilinda kwaajili ya kuwaletea maendeleo.
“Nataka
kufanya kazi kulinda maslahi ya watanzania nimefanyakazi Mamlaka ya
Mapato Tanzania TRA najua ugumu wa kukusanya kodi na kupata mapato, kwa
hiyo nitahakikisha kuwa nailinda kodi ya wananchi kwa wivu mkubwa sana”,
Alisisitiza Kichere.
Kwa upande
wake CAG aliyemaliza muda wake Prof. Mussa Assad alisema kuwa ataendelea
kushirikiana na Ofisi hiyo licha ya kustaafu lakini atakuwepo kwa
wakati ambao atahitajika kutoa msaada kutokana na uzoefu na ujuzi
aliopata kwa muda wa miaka mitano akiwa anatumikia Ofisi hiyo.
“Nataka
nikuambie CAG mpya ukihitaji msaada wa kitu chochote kiwe cha binafsi au
cha kiofisi, ujuzi na uzoefu wa kazi hii niko tayari kushirikiana na
wewe na utapata msaada huo kwa haraka”, Alisema Prof. Assad.
No comments :
Post a Comment