Friday, June 28, 2019

MADAKTARI KUTOKA SHIRIKA LA UMOJA WA MATAIFA (UN) WATEMBELEA TAASISI YA MOYO JAKAYA KIKWETE (JKCI) KWA AJILI YA KUANGALIA HUDUMA ZA MATIBABU YA MOYO NA MISHIPA YA DAMU WANAZOZITOA.


Madaktari kutoka  Shirika la Umoja wa Mataifa (UN)  wakimsikiliza Daktari bingwa wa magonjwa ya moyo Khuzeima Khunbhai kutoka Taasisi ya Moyo  Jakaya Kikwete (JKCI) akiwaeleza jinsi wagonjwa waliolazwa katika chumba cha uangalizi maalum (CCU) wanavyotibiwa.  Madaktari hao walifanya ziara ya kutembelea Taasisi hiyo leo kwa ajili ya kuangalia  huduma za matibabu ya moyo na mishipa ya damu wanazozitoa.

Dk. Adarsh Tiwathia kutoka  Shirika la Umoja wa Mataifa (UN)  akiongea jambo wakati wa kikao na viongozi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakati wa  ziara yao ya  kutembelea Taasisi hiyo leo kwa ajili ya kuangalia  huduma za matibabu ya moyo na mishipa ya damu wanazozitoa.

Madaktari kutoka  Shirika la Umoja wa Mataifa (UN)  wakimsikiliza Daktari bingwa wa magonjwa ya moyo ambaye pia ni Mkurugenzi wa Kurugenzi ya Tiba Shirikishi Delila Kimambo kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) akiwaeleza jinsi duka la dawa la Taasisi hiyo linavyotoa  huduma kwa wagonjwa.  Madaktari hao walifanya ziara ya kutembelea Taasisi hiyo leo kwa ajili ya kuangalia  huduma za matibabu ya moyo na mishipa ya damu wanazozitoa.


Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akiwa katika picha ya pamoja na madaktari kutoka  Shirika la Umoja wa Mataifa (UN) wakati wa  ziara yao ya  kutembelea Taasisi hiyo leo kwa ajili ya kuangalia  huduma za matibabu ya moyo na mishipa ya damu wanazozitoa. (PICHA NA JKCI)

No comments :

Post a Comment