Madaktari
kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa
(UN) wakimsikiliza Daktari bingwa wa
magonjwa ya moyo Khuzeima Khunbhai kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) akiwaeleza jinsi
wagonjwa waliolazwa katika chumba cha uangalizi maalum (CCU) wanavyotibiwa. Madaktari hao walifanya ziara ya kutembelea
Taasisi hiyo leo kwa ajili ya kuangalia huduma za matibabu ya moyo na mishipa ya damu
wanazozitoa.
Dk.
Adarsh Tiwathia kutoka Shirika la Umoja
wa Mataifa (UN) akiongea jambo wakati wa
kikao na viongozi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakati wa ziara yao ya kutembelea Taasisi hiyo leo kwa ajili ya
kuangalia huduma za matibabu ya moyo na
mishipa ya damu wanazozitoa.
Madaktari
kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa
(UN) wakimsikiliza Daktari bingwa wa
magonjwa ya moyo ambaye pia ni Mkurugenzi wa Kurugenzi ya Tiba Shirikishi
Delila Kimambo kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) akiwaeleza jinsi duka
la dawa la Taasisi hiyo linavyotoa
huduma kwa wagonjwa. Madaktari
hao walifanya ziara ya kutembelea Taasisi hiyo leo kwa ajili ya kuangalia huduma za matibabu ya moyo na mishipa ya damu
wanazozitoa.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akiwa
katika picha ya pamoja na madaktari kutoka
Shirika la Umoja wa Mataifa (UN) wakati wa ziara yao ya kutembelea Taasisi hiyo leo kwa ajili ya
kuangalia huduma za matibabu ya moyo na
mishipa ya damu wanazozitoa. (PICHA NA
JKCI)
No comments:
Post a Comment