Pages

Friday, June 28, 2019

MISA TANZANIA, ICNL WAJADILI NA WADAU CHANGAMOTO ZA KISHERIA KWA VYOMBO VYA HABARI


Mkurugenzi wa MISA Tanzania Gasirigwa Sengiyumva akichangia mada katika warsha ya utetezi wa sheria za vyombo vya habari. Geline Fuko (kushoto) akiwasilisha mada wakati wa siku ya pili ya warsha hiyo. Mkurugenzi Mtendaji wa Tanzania Network of Legal Aid Provider Christina Kamili (kulia) akiwasilisha mada wakati wa siku ya pili ya warsha hiyo. Na Mwandishi Wetu Katika kuendeleza hamasa na kutetea uhuru wa kujieleza katika jamii, MISA Tanzania na shirika la utetezi wa sheria na haki za kijamii la ICNL zimewakutanisha wadau mbali mbali katika warsha ya utetezi wa sheria za vyombo vya habari. Warsha hiyo iliyohudhuriwa na wadau mbalimbali wa tasnia ya habari,asasi za utetezi wa haki za binadamu, wanasheria pamoja na wahadhiri wa vyuo vikuu. Warsha hiyo ya siku tatu iliyofanyika mjini Bagamoyo ambayo ni muendelezo wa warsha iliyofanyika mwezi Machi mwaka huu ililenga kuwakutanisha wadau hao kwa lengo la kujadili zaidi namna sheria za vyombo vya habari zinavyo athiri mazingira ya kazi za kiuandishi pamoja na uhuru wa kujieleza. Bw.Aloys Habimana kutoka shirika la kimataifa la utetezi wa haki za kijamii la ICNL akiendesha warsha ya utetezi wa sheria za vyombo vya habari iliyoandaliwa na kuendeshwa na MISA kwa kushirikiana na shirika la kimataifa la utetezi wa haki za kijamii la ICNL. Kadhalika akielezea umuhimu wa uwepo wa sheria rafiki katika kufanya mazingira yawe salama kwa tasnia ya habari,Bw.Aloys Habimana kutoka shirika la kimataifa la utetezi wa haki za kijamii la ICNL lenye makao makuu yake nchini Marekani amesema changamoto ya sheria zisizo rafiki kwa taaluma ya habari na uhuru wa kujieleza ni changamoto sehemu nyingi duniani Afrika ikiwa na mifano halisi. "Pamoja na mazingira haya nawasihi msivunjike moyo wala kukata tamaa, masuala ya kisheria hayabadiliki kwa siku moja yanahitaji kupitia hatua kadhaa na kila jambo linaweza kupatiwa ufumbuzi hasa wadau wote watakaposhirikiana na kujenga hoja zenye ushawishi na tija kwa pande zote", alisisitiza Bw.Aloys. Bi.Lily Liu kutoka shirika la kimataifa la utetezi wa haki za kijamii la ICNL akijadili jambo pamoja na wadau walioshiriki warsha hiyo. Sambamba na hilo Bi.Lily Liu mjumbe kutoka ICNL aliahidi kuwa shirika lao litaendelea kushirikiana na wadau husika katika nyanja zote ili kufanikisha na kutimiza adhma ya kuwa na jamii isiyo na sheria kandamizi zinazoathiri dhana nzima ya uhuru wa kujieleza na vyombo vya habari. Warsha hiyo iliyojikita zaidi katika mfumo wa washiriki kubadilishana mawazo na uzoefu wao wa mazingira ya kazi pamoja na namna hali inavyobadilika na kubanwa kwa uwepo wa sheria zisizojitosheleza. Washiriki warsha hiyo wakijadili baadhi ya sheria na kanuni katika makundi. Mkurugenzi wa Highlands Fm Radio ya Mbeya Bi. Jacqueline Lawrence akiwasilisha mada kwa niaba ya washiriki wenzake Washiriki wa warsha ya utetezi wa sheria za vyombo vya habari iliyoandaliwa na kuendeshwa na MISA kwa kushirikiana na shirika la kimataifa la utetezi wa haki za kijamii la ICNL wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kufungwa kwa warsha hiyo.

No comments:

Post a Comment