Kaimu
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano TCRA, Bw. Semu Mwakyanjala
(watatu kulia), akitoa maelezo kwa mwananchi huyu aliyetembelea banda la
Mamlaka hiyo wakati wa kongamano la uwekezaji Dodoma.
Maafisa
kutoka Idara ya Uhamiaji wakiwahudumia wananchi katika banda la TCRA
ambapo Uhamiaji na taasisi nyingine kama NIDA, Polisi na mitandao ya
simu za viganjani wakiongozwa na TCRA waliendesha zoezi la usajili laini
za simu kwa njia ya alama za vidole biomedtria.
NA
K-VIS BLOG, DODOMA
WAZIRI
Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa ameipongeza Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA)
na wadau wengine kwa kulipa sapoti Kongamano la uwekezaji Dodoma.
Sambamba
na pongezi hizo, Waziri Mkuu Majaliwa pia alimkabidhi cheti cha shukrani Mhandisi
Kiluwa Sepeku kwa niaba ya TCRA.
TCRA
litumia fursa ya kongamano hilo kuendesha zoezi la usajili wa laini za simu kwa
kutumia alama za vidole biometria kwa ushirikiano na taasisi zingine za
serikali zikiwemo Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa NIDA, Idara ya Uhamiaji,
Jeshi la polisi kitengo cha Kuchunguza Uhalifu Mtandaoni pamoja na watoa huduma
za mitandao ya simu za viganjani kama vile TTCL, Airtel, Tigo, Vodacom, Halotel
na Zantel
No comments:
Post a Comment