SERIKALI
ya Ujerumani kupitia Benki yake ya Maendeleo (KfW), imeipatia Tanzania
ruzuku ya Euro milioni 127.7, sawa na sh. bilioni 330, kwa ajili ya
kutekeleza mradi mkubwa wa maji safi na salama kutoka Ziwa Victoria
katika mkoa wa Simiyu.
Makubaliano
ya msaada huo kupitia mikataba miwili yamesainiwa Jijini Dar es Salaam
na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto James kwa niaba
ya Serikali na Mkurugenzi wa Benki ya Maendeleo ya Ujerumani, (KfW)
anayeshughulikia nchi za Afrika Mashariki na Jumuiya ya Ulaya, Dkt.
Klaus Mueller.
Katika
mkataba wa kwanza, kiasi cha Euro 102.7, sawa na shilingi bilioni 265
kimetolewa na Mfuko wa Kimataifa wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabia
Nchi (Green Climate Fund) na mkataba wa pili unahusisha Euro milioni 25,
sawa na sh. bilioni 65 ambazo zimetokelewa na Benki ya Maendeleo ya
UJerumani (KfW).
Mbali
na mradi wa maji wa Simiyu ambao chanzo chake cha maji ni kutoka Ziwa
Victoria, miradi mingine itakayonufaika na msaada huo ni kilimo endelevu
cha umwagiliaji, usafi wa mazingira, maji na malisho ya mifugo na
kuzijengea uwezo taasisi zitakazotekeleza mradi huo hasa mamlaka za maji
katika Wilaya tano za Bariadi, Itilima, Meatu, Busega na Maswa
zitakazonufaika na mradi huo.
"Kutokana
na umuhimu wa mradi huo wa maji, Serikali kwa upande wake itachangia
Euro milioni 40.7 sawa na sh. bilioni 104 na wananchi watakao nufaika na
mradi huo watachangia Euro milioni 1.5 sawa na sh. bilioni 3.8 na
kufanya gharama za mradi mzima kufikia zaidi ya Euro milioni 171 sawa na
zaidi ya sh. bilioni 446" alisema Bw. Doto James
Aliishukuru
Serikali ya Ujerumani kupitia Mfuko wake wa Kimataifa wa kukabiliana na
athari za mabadiliko ya tabianchi (GCF) na Benki ya Maendeleo ya
Ujerumani (KfW) kwa kutoa kiasi hicho kikubwa cha fedha kitakachotumika
kutekeleza mradi huo utakachukua miaka mitano hadi kukamilika kwake.
"Katika
kipindi cha miaka mitatu Serikali ya Ujerumani imeipatia Tanzania
zaidi ya Euro 202.8 sawa na shilingi bilioni 518.5 kwa ajili ya
kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo katika sekta za afya, nishati,
uhifadhi wa maliasili, udhibiti wa fedha za umma na Ofisi ya Taifa ya
Ukaguzi" alisisitiza Bw. James
Kwa
upande wake Mkurugenzi wa Benki ya KfW amesema kuwa hii ni mara ya
kwanza kwa Mfuko wa Kimataifa kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi
kutoa kiasi kikubwa cha fedha cha Euro milioni 102.7 kwa mkupuo katika
nchi za kiafrika tangu mfuko huo uanzishwe.
"Tunaamini
kuwa zaidi ya watu 500,000 watanufaika na mradi huu wa maji kutoka Ziwa
Victoria unaohusiana na kukabiliana na changamoto za mabadiliko ya
tabianchi kwa kutuhifadhi vyanzo vya maji, usafi wa mazingira, kuendesha
kilimo bora chenye kuhifadhi mazingira" aliongeza Dkt. Mueller.
Akizungumza
katika hafla hiyo, Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji, Prof. Kitila Mkumbo,
amempongeza Rais Dkt. John Pombe Magufuli na uongozi wa Wizara ya Fedha
na Mipango kwa kuipatia Wizara yake zaidi ya shilingi trilioni 3 katika
kipindi kifupi cha miaka mili kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali
ya maji inayoendelea kujengwa nchini kote.
Alitaja
sababu za mkoa wa Simiyu kunufaika na msaada huo kuwa ni mkoa
unaokabiliwa na hali mbaya ya hewa ukiwemo ukame na kwamba mradi huo
utawawezesha wananchi kuhimili mabadiliko ya tabianchi na kwamba katika
ukanda huo wa Ziwa kutakuwa na miradi ya maji yenye thamani ya zaidi ya
shilingi trilioni 1.2 itakayokuwa inatekelezwa.
Naye
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji, Mhe.
Mahamoud Mgimwa amesema Bunge litahakikisha linausimamia mradi huo
utekelezwe kwa wakati kwa sababu Serikali imedhamiria kwa dhati kuona
kwamba wananchi wanapata maji safi na salama kwa asilimia 95 ifikapo
mwaka 2025.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto James (kulia) na Mkurugenzi wa Benki ya Maendeleo ya Ujerumani (KFW) katika nchi za Afrika Mashariki na Jumuiya ya Ulaya Dkt. Klaus Mueller, wakionesha mkataba wa msaada wa Euro
milioni 127.7 sawa na Sh. bilioni 330 kwa ajili ya kugharamia mradi wa
maji katika Mkoa wa Simiyu baada ya kusainiwa, katika ukumbi wa Wizara
ya Fedha na Mipango Jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto James (kulia) na Mkurugenzi wa Benki ya Maendeleo ya Ujerumani (KFW) katika nchi za Afrika Mashariki na Jumuiya ya Ulaya Dkt. Klaus Mueller, wakibadilishana mkataba wa ruzuku/msaada wa Euro
milioni 127.7 sawa na Sh. bilioni 330 kwa ajili ya kugharamia mradi wa
maji katika Mkoa wa Simiyu, hafla iliyofanyika katika ukumbi wa Wizara
ya Fedha na Mipango Jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto James (kulia) na Mkurugenzi wa Benki ya Maendeleo ya Ujerumani (KFW) katika nchi za Afrika Mashariki na Jumuiya ya Ulaya Dkt. Klaus Mueller, wakisaini Mkataba wa ruzuku ya Euro milioni 127.7 sawa na Sh. bilioni 330 kwa ajili ya kugharamia mradi wa
maji kutoa Ziwa Victoria kupitia mradi wa kukabiliana na athari za
Mabadiliko ya Tabia nchi katika Mkoa wa Simiyu, hafla hiyo ilifanyika
katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dar es Salaam.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto James (kulia), akieleza
kuwa licha ya msaada wa Sh. bilioni 330 kutoka Benki ya Maendeleo ya
Ujerumani (KFW), kwa ajili ya mradi
wa maji ya Ziwa Victoria katika Mkoa wa Simiyu, Serikali ya Tanzania
itachangia kiasi cha Euro milioni 40.7 ambayo ni sawa na Sh. 104.1
kutokana na umuhimu wa mradi huo.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Maji, Prof. Kitila Mkumbo, akieleza kuwa Euro milioni
127.7 sawa na Sh. bilioni 330 zilizotolewa na Benki ya Maendeleo ya
Ujerumani (KFW) zitawanufaisha
wananchi wa Mkoa wa Simiyu kupitia miradi ya maji, kilimo cha
umwagiliaji na usafi wa mazingira, wakati wa hafla ya kusaiiniwa kwa
msaada wa fedha hizo katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango Jijini
Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa
Kamati ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji, Mhe. Mahamoud Mgimwa (Mb),
akieleza kuwa msaada wa Sh. bilioni 330 zilizotolewa kwa ajili ya miradi
ya kukabiliana na mabadiliko ya Tabia nchi utasaidia kuondoa malalamiko
ya mda mrefu ya wabunge wa wilaya zitakazonufaika na mradi huo kuhusu
ukosefu wa maji Mkoa wa Simiyu.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto James (katikati) na Mkurugenzi wa Benki ya Maendeleo ya Ujerumani (KFW) katika
nchi za Afrika Mashariki na Jumuiya ya Ulaya Dkt. Klaus Mueller (wa
pili kulia), wakiwa katika picha ya pamoja na wajumbe kutoka Tanzania na
Benki ya KfW ya Ujerumani baada ya kukamilika kwa hafla ya kusainiwa
mkataba wa msaada wa Euro milioni 127.7 sawa na Sh. bilioni 330 kwa ajili ya kugharamia mradi wa maji kutoa Ziwa Victoria kwenda Mkoa wa Simiyu.
Mkuu
wa mkoa wa Simiyu Antony Mtaka akizungumza Wakati wa uzinduzi wa
kampeni ya Jiongeze Tuwavushe salama ilyofanyika mkoni hapo.
Wadau wakiwa kwenye uzinduzi wa Jiongeze tuwavushe salama iliyofanyika mkoani Simiyu.
Wadau wakiwa katika uzinduzi wa Kampeni ya Jiongeze tuwavushe salama Mkoani Simiyu.
Na.Vero Ignatus.
Baadhi ya akina mama katika Halmashauri ya mji Bariadi hawana maamuzi ya kwenda hospitali kupata huduma za afya, wakisubiri ruhusa kutoka Kwa waume wao au wakwe zao.
Hayo yamesemwa na Mratibu wa Afya ya Mama na Mtoto katika halmashauri ya Mji wa Bariadi, Frida Buyoga katika uzinduzi Wa kampeni ya ' Jiongeze Tuwavushe Salama katika mkoa wa Simiyu, amesema ukosefu huo wa kutoa maamuzi umepelekea wengi wao kupoteza Maisha Kwa sababu ya kuchelewa kufika vituo vya Afya.
Ukosefu wa maamuzi pia unapelekea baadhi ya akina mama hao kushindwa kupanga uzazi wa mpango mpaka wawaulize waume zao.
Buyoga, amesema hali hii imepelekea vifo vya vya akina mama 14 , kati ya 120 waliochelewa kufika vituo vya afya kwa sababu mbalimbali mwaka jana.
Licha ya akina mama hao kufariki, watoto wao waliokuwa bado hawajazaliwa (tumboni) walikutwa hawachezi (wamefariki) baada ya kuchelewa kufika vituo vya Afya.
Amesema miongoni mwa sababu nyingine zinazopelekea baadhi ya akina mama kuchelewa kufika vituo vya Afya ni pamoja na umbali Wa baadhi ya vituo vya Afya, ambapo baadhi yao hulazimika kusafiri hadi kilometa 30 kwenda katika vituo vya Afya.
" Jitihada Kubwa zimefanyika kusaidia wajifungue Salama, ikiwemo ujenzi Wa zahanati na vituo vya Afya unaofanywa na serikali na wadau wa maendeleo.
Amesema katika halmashauri ya mji wa Bariadi, akina mama wastani 15-22 wanajifungua kila wiki , ikiwa ni ongezeko Kwa wanaokwenda kujifungua katika vituo vya Afya.
" Baadhi ya akina mama wamekuwa wakijifungua Nyumbani, lakini baada ya kuwapa elimu, wengi wao sasa hivi wanakwenda vituo vya Afya kujifungua na kupata huduma Kwa ajili yao na watoto wao, anasema Buyoga.
Amesema uzinduzi Wa kampeni ya 'Jiongeze Tuwavushe Salama' utasaidia sana kuelimisha akina mama kwenda katika vituo vya Afya, kujua Afya zao na kufuatilia chanjo zote muhimu, ili kujilinda wao na watoto wao.
No comments :
Post a Comment