Naibu
Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu ( wa pili
kulia) akioneshwa michoro ya mapangoni na Askari Wanyamapori iliyochorwa
zaidi ya miaka 1000 iliyopita na kabila la Wasandawe ambayo ni miongoni
mwa vivutio vya Utalii wakati alipotembelea mara baada ya kuzungumza
na watumishi wa Pori la Akiba la Swagswaga katika ziara yake ya kikazi
wilayani Chemba jijini Dodoma. Wa kwanza kulia ni Naibu Kamishna wa
Uhifadhi wa TAWA, Mabula Misungwi.
Naibu
Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu (wa tatu kulia)
akiangalia baadhi michoro ya mapangoni iliyochorwa zaidi ya miaka 1000
iliyopita na kabila la Wasandawe ambayo ni miongoni mwa vivutio vya
Utalii wakati alipotembelea mara baada ya kuzungumza na watumishi wa Pori la Akiba la Swagswaga katika ziara yake ya kikazi wilayani Chemba jijini Dodoma. Wa kwanza kulia ni Meneja wa Pori hilo, Alex Choya.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu akizungumza na watumishi wa Pori la Akiba la Swagaswaga mara baada ya kutembelea michoro ya mapangoni iliyochorwa zaidi ya miaka 1000 na kabila la Wasandawe katika wilaya ya Chemba mkoani Dodoma
Pia,
amewataka wananchi kuwachukulia Wahifadhi hao kama rafiki wa umma na
watendaji waliotumwa na Serikali kulinda Maliasili kwa niaba yao.
Akizungumza
na Watumishi wa Pori la Akiba la Swagaswaga katika wilaya ya Chemba
jijini Dodoma, Mhe. Kanyasu amesema Wahifadhi wamepewa jukumu la
kulinda hifadhi za Taifa na wamekuwa wakifanya kazi nzuri ya kuifanya
Tanzania iendelee kuwa na maeneo mazuri yaliyohifadhiwa.''Sisi
ni wa moja hakuna haja ya kujengeana uhasama kati yetu, Wananchi
wafuate sheria za Uhifadhi na Wahifadhi fuateni sheria wakati
mnapokabaliana na Wananchi'' amesisitiza Kanyasu.Amesema
Wahifadhi wa Wanyamapori na Misitu wanazilinda rasilimali hizo kwa
ajili wote, vitu kama mvua, hali ya hewa safi pamoja na mvua ni moja ya
faida za moja kwa moja zinazopatikana kutokana na maeneo yaliyohifadhiwa
vizuri.
Amesema
Wahifadhi hao wameajiriwa kwa mujibu wa sheria hivyo hutekeleza
majukumu yao kwa kuzingatia maadili ya kazi zao na pale wanapokiuka
sheria mamlaka zinazohusika huwachukulia hatua.
“Sisi
kama Wizara tunaamini kwamba wahifadhi wetu wanafanya kazi nzuri, pale
ambapo wamekuwa wakilaumiwa kwa kuwapiga na kuwanyanyasa watu kwa namna
yoyote ile tumetuma Tume maalum kuchunguza na kuchukua hatua” Amesema
Mhe,
Kanyasu amesema uchunguzi unapofanyika na ikathibitika kuwa tukio
lililofanyika halikuongozwa na matumizi ya sheria na kuwepo kwa haki
wizara imekua ikichukua hatua.
Ameeeleza
kuwa Wahifadhi ni watu muhimu saba kwa vile bila wao hakuna uhifadhi
unaoweza kuendelea nchini akibainisha kuwa baadhi ya watu wamekuwa
wakipinga juhudi za uhifadhi kwa kuwatetea watu wanaovunja sheria.
Kuna
watu wanatamani kuona misitu na wanyamapori wote tunawamaliza ili
wapate maeneo ya malisho na kilimo, Nawambieni tukithubutu kufanya hivyo
huu ndo utakuwa mwisho wetu wa maisha" Amesisitiza Mhe.Kanyasu
Amesema
yapo madhara makubwa yanayoweza kutokea kama hakutakuwa na uhifadhi
imara ikiwemo maeneo mengi ya nchi kugeuka kuwa jangwa kutokana na
uharibifu wa misitu, ukosefu wa mvua, ukosefu wa maji, chakula na
ukosefu wa hewa safi.
Kwa
upande wake, Meneja wa Pori la Akiba la Swagaswaga, Alex Choya amesema
kuwa kumekuwa na tuhuma za vitendo vya ukatili dhidi ya raia
vinavyofanywa na baadhi ya askari wa hifadhi za Taifa na kutoa wito kwa
wananchi wote wenye ushahidi na taarifa juu ya vitendo hivyo
kuziwasilisha ili hatua stahiki zichukuliwe.
Amesisitiza
kuwa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) hairuhusu
askari kufanya vitendo vya ukatili na unyanyasaji dhidi ya raia badala
yake imekua ikiwahamasisha wananchi kushiriki kikamilifu katika ulinzi
wa rasilimali zinazowazunguka.
No comments :
Post a Comment