Friday, May 3, 2019

MABALOZI WASHIRIKI KATIKA KILELE CHA SIKU YA UHURU WA HABARI DUNIANI ILIYOADHIMISHWA KITAIFA JIJINI DODOMA


 Msemaji Mkuu wa Serikali ambaye pia ni Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Habari Malelezo, Dkt. Hassan Abass, (wapili kulia mbele), akiongozana na Kaimu Balozi wa Marekani nchini, Mhe.Bi. Immi Patterson (watatu kushoto) na Balozi wa Uingereza nchini, Me. Sarah Cooke, wakitoka kwenye ukumbi w ahoteli ya Morena jijini Dodoma leo Mei 3, 2019 mara baada ya kuungana na wanatasnia ya habari nchini, kuadhimisha siku ya uhuru wa habari (World Press Freedom jijini Dodoma
 Kaimu Balozi wa Marekani nchini, Mhe.Bi. Immi Patterson akihutubia kwenye kilele cha siku ya Uhuru wa Habari (World Press Freedom Day), kwenye hoteli ya Morena jijini Dodoma leo Mei 3, 2019.
Kaimu Balozi wa Marekani nchini, Mhe.Bi. Immi Patterson(kushoto), akitembelea mabanda ya maonesho ya shughuli za wanahabari mara baada ya kuhutubia katika kilele cha siku ya uhuru wa vyombo vya habari duniani kwenye hoteli ya Morena jijini Dodoma Mei 3, 2019. Wapili kushoto Kaimu Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri (TEF), Bw. Deodatus Balile, na Dkt. Hassan Abass, Msemaji Mkuu wa  Serikali ambaye pia ni Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Habari Malelezo. 

No comments :

Post a Comment