Monday, April 1, 2019

Udhamini wa Benki ya NBC Wafanikisha Jukwaa la Tafakuri


01
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangala, akikabidhi cheti kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC, Theobald Sabi (kulia), kwa kutambua mchango wa benki hiyo kama mdhamini mkuu katika uzinduzi wa Jukwaa la Tafakuri jijini Dar es Salaam juzi.

02.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangala (kushoto), akizungumza katika uzinduzi wa Jukwaa la Tafakuri jijini Dar es Salaam juzi. Uzinduzi huo ulidhaminiwa na Benki ya NBC.
03
Taswira ya kwenye video ikimuonyesha mmoja wa wanahabari nguli nchini, Jenerali Ulimwengu wakati ikionyesha makala kuhusu urithi wa Mwalimu Nyerere ikiwa ni moja ya matukio wakati wa uzinduzi rasmi wa Jukwaa na Tafakuri katika Ukumbi wa Cinemax, jijini Dar es Salaam juzi.
04
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangala (kushoto), akishikana mikono na Mkurugenzi Mtendaji wa NBC, Theobald Sabi mara baada ya kumalizika shughuli za uzinduzi huo.  
05
Meneja Mawasiliano wa NBC, William Kallaghe (kushoto), akipokea cheti kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo, Theobald Sabi mara baada ya kukabidhiwa na Waziri wa Maliasili na Utalii. NBC ni mdhamini mkuu wa Jukwaa la Tafakuri  lenye lengo la kuchagiza vijana kuwa wazalendo na vilevile kufufa tunu za utaifa, na ambalo litaandamana na shughuli mbalimbali zenye lengo la kuchagiza kufufuka na kushamiri kwa moyo wa uzalendo nchini.

No comments :

Post a Comment