Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk.
Hamisi Kigwangala, akikabidhi cheti kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya
NBC, Theobald Sabi (kulia), kwa kutambua mchango wa benki hiyo kama
mdhamini mkuu katika uzinduzi wa Jukwaa la Tafakuri jijini Dar es Salaam
juzi.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk.
Hamisi Kigwangala (kushoto), akizungumza katika uzinduzi wa Jukwaa la
Tafakuri jijini Dar es Salaam juzi. Uzinduzi huo ulidhaminiwa na Benki
ya NBC.
Taswira ya kwenye video
ikimuonyesha mmoja wa wanahabari nguli nchini, Jenerali Ulimwengu wakati
ikionyesha makala kuhusu urithi wa Mwalimu Nyerere ikiwa ni moja ya
matukio wakati wa uzinduzi rasmi wa Jukwaa na Tafakuri katika Ukumbi wa
Cinemax, jijini Dar es Salaam juzi.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk.
Hamisi Kigwangala (kushoto), akishikana mikono na Mkurugenzi Mtendaji
wa NBC, Theobald Sabi mara baada ya kumalizika shughuli za uzinduzi huo.
Meneja Mawasiliano wa NBC, William
Kallaghe (kushoto), akipokea cheti kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa
benki hiyo, Theobald Sabi mara baada ya kukabidhiwa na Waziri wa
Maliasili na Utalii. NBC ni mdhamini mkuu wa Jukwaa la Tafakuri lenye
lengo la kuchagiza vijana kuwa wazalendo na vilevile kufufa tunu za
utaifa, na ambalo litaandamana na shughuli mbalimbali zenye lengo la
kuchagiza kufufuka na kushamiri kwa moyo wa uzalendo nchini.
No comments:
Post a Comment