Pages

Monday, April 1, 2019

SERIKALI KUFUNGA RADA NYINGINE MBILI ZA HALI YA HEWA MKOA WA MBEYA NA KIGOMA


Mkurugenzi wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), Dk. Agness Kijazi (kushoto) akisaini mkataba wa ununuzi wa Rada mbili za mamlaka hiyo na mwakilishi wa Kampuni ya Enterprise Electronics Corporation (ECC), Edwin Kasanga ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Infratech Ltd (T) leo jijini Dar es Salaam. Tukio hilo limeshuhudiwa na Naibu Waziri Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Eng. Atashasta Nditiye (katikati waliosimama) pamoja na Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya TMA, Dk. Buruhani Nyenzi (kushoto nyuma).
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), Dk. Agness Kijazi (kushoto) akisaini mkataba wa ununuzi wa Rada mbili za mamlaka hiyo na mwakilishi wa Kampuni ya Enterprise Electronics Corporation (ECC), Edwin Kasanga ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Infratech Ltd (T) leo jijini Dar es Salaam. Tukio hilo limeshuhudiwa na Naibu Waziri Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Eng. Atashasta Nditiye (wapili kulia waliosimama) pamoja na Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya TMA, Dk. Buruhani Nyenzi (wa pili kushoto nyuma). Wengine ni wanasheria wa pande zote, Emmanuel Ntenga wa TMA (kushoto) na Queen Allen wa ECC.

Mkurugenzi wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), Dk. Agness Kijazi (kushoto) wakibadilishana nakala za mkataba huo na Mwakilishi wa Kampuni ya Enterprise Electronics Corporation (ECC), Edwin Kasanga ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Infratech Ltd (T) leo jijini Dar es Salaam mara baada ya kutiliana saini. Anayeshuhudia katikati ni Naibu Waziri Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Eng. Atashasta Nditiye.

Mkurugenzi wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), Dk. Agness Kijazi (kushoto) pamoja na Mwakilishi wa Kampuni ya Enterprise Electronics Corporation (ECC), Edwin Kasanga (kulia)  wakionesha nakala za mikataba leo jijini Dar es Salaam mara baada ya kutiliana saini ununuzi wa Rada mbili za hali ya hewa zitakazofungwa eneo la Kawetere katika Halmashauri ya Jiji la Mbeya na eneo la Nyamoli katika barabara ya kuelekea Bulombora, Kigoma na hivyo kuifanya Tanzania kuwa na jumla ya mtandao wa rada tano (5).

Naibu Waziri Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Eng. Atashasta Nditiye (katikati) akizungumza kwenye hafla ya kutiliana saini ununuzi wa Rada mbili za hali ya hewa zitakazofungwa eneo la Kawetere katika Halmashauri ya Jiji la Mbeya na eneo la Nyamoli katika barabara ya kuelekea Bulombora, Kigoma na hivyo kuifanya Tanzania kuwa na jumla ya mtandao wa rada tano (5). 

Mkurugenzi wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), Dk. Agness Kijazi akijibu maswali ya wanahabari mara baada ya kusaini mkataba huo. Kulia ni Naibu Waziri Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Eng. Atashasta Nditiye.

SERIKALI ya awamu ya tano
imejizatiti katika kuhakikisha huduma za hali ya hewa nchini zinakuwa za
viwango vya kimataifa na za usahihi wa hali ya juu. Katika kufanikisha hili
Serikali ya awamu ya tano iliahidi kuendelea kuongeza mtandao wa Rada za hali
ya hewa ili kufikia Rada saba (7) zinazohitajika kwa nchi nzima.
 
Serikali kupitia Mamlaka
ya Hali ya Hewa Tanzania, imesaini mkataba wa ununuzi wa Rada mbili za hali ya
hewa zitakazofungwa eneo la Kawetere katika Halmashauri ya Jiji la Mbeya na
eneo la Nyamoli katika barabara ya kuelekea Bulombora, Kigoma na hivyo kuifanya
Tanzania kuwa na jumla ya mtandao wa rada tano (5).
 
Ikumbukwe kuwa tayari Mamlaka
imeishafunga rada mbili za hali ya hewa huko Kiseke Mwanza na Bangulo Dar es
Salaam pia imeanza utaratibu wa ufungaji wa Rada Mtwara. Hii inaifanya Tanzania
kuwa Taasisi bora kwa uangazi wa wa hali ya hewa kwa njia ya Rada katika ukanda
wa Afrika Mashariki na Kati.
 
Ununuzi wa Rada hizi mbili (ya nne na ya tano) kwa ajili ya Mbeya
na Kigoma umegharimu kiasi cha Tshs. 5,715,971,148.45 (USD 2,497,125) kwa
kila moja na pia utengenezaji na ufungaji wa rada zote mbili utachukua muda wa
miezi kumi na nne hadi kukamilika kwake.
 Mtengenezaji wa
Rada hizo ni Enterprise Electronics Corporation (ECC).
 
Rada
hizi zina uwezo wa kuona hadi kilometa za mkato 450 (Aerial distance) huku
zikizunguka (radius distance) na uwezo halisia wa kuona mpaka matone madogo
sana ya mvua ni kilometa za mkato 250.
 
Rada za hali ya hewa ni moja ya mitambo
inayotumika kufanya uangazi wa hali ya hewa wa masafa marefu. Mitambo hii
husaidia katika kukusanya data za hali ya hewa zinazoonesha uhalisia wa anga
kipindi Radar inapozunguka. Rada inasaidia;
·
Kujua
kwa wakati maeneo yenye mvua, aina ya mawingu yaliyopo na wakati mwingine hata
kujua ni kiasi gani cha mvua kinachotarajiwa.
  • Kufuatilia
    maeneo yenye mvua kubwa na za mawe zinazoambatana na radi na upepo mkali
    hivyo kuweza kutoa tahadhari kwa muda muafaka.
  • Kufuatilia
    muelekeo wa mifumo inayosababisha hali mbaya ya hewa (mvua za mawe, upepo
    mkali na dhoruba).
  • kufuatilia
    vimbunga baharini kadri ya upeo wake na hivyo kuweza kutoa tahadhari
    kutokana na mwenendo wa vimbunga hivyo.
  • Kufuatilia
    upepo unaoweza kuleta madhara kwa usalama wa usafiri wa anga (wind shear)
    na
  • Kutoa ushauri
    kwa watumiaji wa huduma za hali ya hewa ili wachukue tahadhari wakati wa shughuli
    zao kiuchumi na kijamii.
  • Kusaidia kutoa
    utabiri wa muda mfupi na wakati wa hali mbaya ya hewa.
Kwa kumalizia
napenda kuwashukuru kwa ushirikiano wenu katika kusambaza taarifa za hali ya
hewa na napenda kutoa wito kwa wananchi wote kutoa ushirikiano katika kulinda
na kutunza mitambo hii ya Rada pamoja na vifaa vyote vya hali ya hewa kwa
manufaa ya Taifa letu.
Imetolewa na:
Ofisi ya Uhusiano
Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA)

No comments:

Post a Comment