Tuesday, April 2, 2019

TGNP MTANDAO YAPANIA KUFANYA MAKUBWA KATIKA BAJETI YA MWAKA 2019-2020


AAAA
Mkurugenzi mtendaji wa bodi TGNP maendeleo, Lilia Liundi akizungumza na wadau mbalimbali katika mjadala wa bajeti ya mwaka 2019-2020
AAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAA
Wadau mbalimbali wakifuatilia mjadala wa bajeti ya mwaka 2019-2020
…………………….
NA EMMANUEL MBATILO
TGNP Mtandao kushirikiana na wadau mbalimbali hapa nchini wameandaa mjadala kabla ya bajeti kuu 2019-2020 la dhumuni la ... kutathimini utekelezaji wa mpango wa taifa wa pili na hatua iliyofikia nchini katika kutatua usawa wa jinsia na uwezeshaji wa wanawake.
Akizungumza na wanahabari jijini Dar es Salaam, mwenyekiti wa bodi TGNP Mtandao, Asseny Muro amesema mojawapo ya mikakati inayotumiwa na TGNP Mtandao katika kuleta maendeleo katika jamii hasa usawa wa jinsia na haki za jamii ni uchambuzi wa sera na mipango na bajeti kwa walengwa wa jinsia.
“Shirika limerasmisha programu ya uchambuzi wa bajeti kwa baadhi ya almshauri, wizara na bajeti ya taifa na hii imekuwa ni programu kubwa ya shirika katika kutengeneza taarifa zitakazoendelea kutumika katika kudai na kuhamasisha utekelezaji wa sera na bajeti yenye mlengwa wa jinsia”. Amesema Asseny.
Aidha Asseny amesema kuwa mwaka huu TGNP imeratibu jukwaa la kuwashirikisha wadau mbalimbali kujadili na kutoa mapendekezo yao yatakayowezesha uboreshaji na utekelezaji wabajeti ya mwaka 2019 na 2020 kwa mlengwa wa jinsia.
“Kumuwezesha kila mmoja kutathimini utekelezaji wa maswala ya jinsia kwa kuangalia mikataba na maadhimio mbalimbali kama vile dira ya maendeleo ya taifa 2025”. Ameongeza Asseny.
Hata hivyo kwa upande wa mkuu wa idara ya utafiti na uchambuzi wa sera TGNP mtandao, Happiness Maruchu amesema kuwa lengo kuu la bajeti hiyo ni kuhakikisha linainua makundi yaliyopo chini kwa kutenga rasirimali za kutosha katika kushughulikia changamoto zao.
“Tunaona msisitizo mkubwa wa bajeti tangu mwaka 2016 ipo sana kwenye ujenzi wa miundombinu na sisi kwa mtazamo wetu si kwamba ujenzi wa miundombinu ni kitu kibaya hapana tunahitaji kuchochea uchumi kwasababu uchumi ukikuwa tunatengeneza ajira”. Amesema Happiness.

No comments :

Post a Comment