Na.Alex Sonna,Dodoma
BUNGE la Jamuhuri ya Muungano wa
Tanzania limeazimia kwa kauli moja na kutoa hatia kwa Mkaguzi na
Mdhibiti Mkuu wa hesabu za Serikali(CAG), Profesa Mussa Assad na kukataa
kufanya naye kazi na kushirikiana naye katika jambo lolote.
Aidha limetoa adhabu kwa
Mbunge wa Kawe, Mhe.Halima Mdee kwa kusimamishwa kuhudhuria mikutano
miwili ya Bunge mpaka bunge la mwezi wa tisa (Septemba) ambapo adhabu
yake itamalizika Kamati ya kudumu ya bunge haki, maadili na madaraka ya
bunge imetoa taarifa yake kuhusiana na sakata hilo.
Mwenyekiti wa kamati Emmanuel
Mwakasaka,amesoma taarifa hiyo ambapo amesema kuwa Kamati
imejiridhisha pasina shaka kuwa kauli aliyoitoa CAG Asadi akiwa nchini
Marekani akihojiwa na katika kituo cha redio cha idhaa ya kiswahili
umoja wa mataifa zililenga kuridharirisha bunge la Tanzania na hivyo
kamati imesisitiza haiko tayari kufanya tena kazi na CAG Asadi.
Mwakasaka amefafanua kuwa, kwa
kitendo cha Profesa Assad kushikilia msimamo wa kauli yake na kukataa
kuomba radhi ni dharau kubwa kwa bunge na taifa kwa ujumla, hivyo
wanasitisha kufanya naye kazi wala kushirikiana naye kwa chochote.
Kuhusu azimio la Mdee, amesema
alipohojiwa na kamati alikiri kuunga mkono kauli iliyotolewa na Profesa
asadi licha ya kuwa yeye hakulenga kulidhalilisha bunge wala kudharau
muhimili huo.
Amesema hata hivyo mdee hakuonyesha kujutia kauli yake ya kuunga mkono na wala hakuomba radhi mbele ya kamati.
Hata hivyo Mwenyekiti amesema
kuwa hiyo ni mara ya nne kwa Mbunge huyo kuitwa mbele ya kamati hiyo
kuhojiwa makosa mbalimbali ikiwemo kudharau kiti cha Spika na mara zote
tatu alipewa adhabu.
Amesema Januari 2019 baada ya
kamati kumhoji walijiridhisha ana hatia na kuazimia kumpa adhabu ya
kutohudhuria vikao viwili vya Bunge kwa maana ya kikao chote cha Bunge
hili la bajeti kinachoendelea na kikao cha Septemba mwaka huu.
No comments :
Post a Comment