Monday, April 1, 2019

TAARIFA KWA UMMA KUHUSU UTEUZI WA WAJUMBE WA BODI YA URATIBU WA MASHIRIKA YASIYO YA KISERIKALI

index
Kufuatia Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Joseph Magufuli kumteua Dkt. Richard Faustine Sambaiga kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Uratibu wa
Mashirika Yasiyo ya Kiserikali; Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mheshimiwa Ummy A. Mwalimu (Mb.), kwa mamlaka aliyonayo chini ya Kifungu cha 1(1) (b) na (c) cha Jedwali la Sheria ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Na. 24 ya mwaka 2002 (kama ilivyofanyiwa marekebisho mwaka 2005), amewateua wafuatao kuwa wajumbe wa Bodi ya Uratibu wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali:
  1. Bi. Marlin Leonce Komba
  2. Bw. Ally Said Nzory
  3. Bw. Klaus Mohamed Kilamla
  4. Dkt. Zena Mnasi Mabeyo
  5. Dkt. Alli Abushiri Shomari Mcharo
  6. Bw. Ismail Abdulnur Suleiman
  7. Bi. Mary Paul Dafa
  8. Bw. Milton Nestory Lutabana
  9. Bw. Hassani Samli
Uteuzi wa wajumbe hao umeanza tarehe 23 Machi, 2019.

No comments :

Post a Comment