Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus
Nyongo (Mbele Kushoto) akiwa na Naibu Waziri wa Maliasili wa China Dkt,
Zhong Ziran (Kulia) pamoja na wajumbe walioambatana nao katika kikao
kilichofanyika katika ukumbi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwl. JK
Nyerere Jana.
Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus
Nyongo (Mbele Kushoto) akiwa na Naibu Waziri wa Maliasili wa China Dkt,
Zhong Ziran (Kulia) pamoja na wajumbe walioambatana na Wajumbe
alioambatana nao kutoka China wakifuatilia jambo katika kikao
kilichofanyika katika ukumbi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwl. JK
Nyerere Jana.
Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus
Nyongo (Kushoto- waliokaa) akiwa na Naibu Waziri wa Maliasili wa China
Dkt, Zhong Ziran (Kulia) pamoja na wajumbe walioambatana nao kutoka
pande hizo mbili mara baada ya kumaliza kikao kilichofanyika mara baada
ya ugeni kutoka China kuwasili.
……………………….
Nuru Mwasampeta na Tito Mselem
Naibu Waziri wa Madini, Stansilaus
Nyongo jana tarehe 28 April, 2019 amepokea ujumbe ulioongozwa na Naibu
Waziri wa Maliasili wa Jamhuri ya Watu wa China waliofika kwa ajili
ya
kujadili maeneo ya kushirikiana katika sekta ya madini baina ya nchi
hizo mbili yaani Tanzania na China.
Akizungumza wakati akifungua kikao
cha majadiliano baina ya nchi hizo mbili, Nyongo aliwahakikishia wageni
hao kuwa Serikali ya Awamu ya Tano imeweka mazingira mazuri ya kuwekeza
nchini kupitia sekta ya Madini na kuwataka kutosita kutembelea maeneo
mbalimbali ili kujionea fursa zilizopo na kuwekeza nchini Tanzania.
Nyongo amewadhihirishia wageni hao
uwepo wa sera na sheria zisizokandamiza upande wowote baina ya
wawekezaji, wananchi na Serikali na hivo kuzifanya pande zote kunufaika
na rasilimali na uwekezaji unaofanyika katika sekta ya madini.
Aidha, Nyongo amebainisha kuwa
ushirikiano baina ya Tanzania na China ni wa muda mrefu ikiwa ni
takribani miaka 50 na kufika kwa ujumbe huo kunabainisha wazi kuwa
urafiki na ukaribu baina ya nchi hizo hauna mashaka.
Akizungumza na waandishi wa Habari
mara baada ya mkutano huo, Nyongo alisema wataalamu kutoka China
wamekuja kuunganisha nguvu ya pamoja na watanzania ili kuweza kusaidiana
katika kufanya tafiti za kina katika kujua kiasi cha madini yaliyopo,
namna nzuri ya kuvuna madini hayo pamoja na namna ya kuyaongezea thamani
madini yaliyopo nchini kabla ya kuyasafirisha nje ya nchi.
Pia, Nyongo amebainisha kuwa China
ipo tayari kuleta wataalamu katika masuala ya madini watakaojikita
katika kufanya shughuli za uchimbaji wa madini.
Naibu Waziri Nyongo amebainisha
kuwa ujio wa ujumbe kutoka China utasaidia kuweka makubaliano ya pamoja
baina ya Taasisi ya Utafiti na Jiolojia Tanzania na Taasisi ya Jiolojia
na utafiti ya nchini China katika kusimamia masuala ya utafiti wa madini
katika maeneo ambayo hayajafikiwa.
Zaidi ya hayo Nyongo
amewadhihirishia wageni hao uwepo wa mazingira mazuri na rafiki ya
uwekezaji yanayotokana na uwepo wa sera na sheria zisizokandamiza upande
wowote baina ya wawekezaji na Serikali na kuwataka kutosita kuja
kuwekeza nchini.
Kwa upande wake Kaimu Mtendaji
Mkuu wa Taasisi ya Utafiti na Jiolojia nchini Bi Yourghbert Myumbilwa
amesema ushirikiano huo utaleta manufaa makubwa kwani uzoefu wa China
katika masuala ya utafiti ni mkubwa hivyo itawawezesha watumishi wa
taasisi hiyo kupata uelewa mkubwa katika kutekeleza majukumu yao.
Akizungumzia ujio wa ujumbe wake
nchini, Naibu Waziri wa Maliasili wa China Dkt. Zhong Ziran amesema ni
kuweza kujadili na kukubaliana juu ya maeneo ya kushirikiana baina ya
Tanzania na China kupitia maliasili madini inayopatikana nchini.
Ushirikiano huu baina ya Taasisi
ya Utafiti na Jiolojia nchini na Taasisi ya Utafiti wa Jiolojia nchini
China ni matokeo ya kikao kilichofanyika mwezi Desemba, 2018 baina ya
aliyekuwa Waziri wa Madini, Angellah Kairuki na Waziri wa Maliasili wa
China kilichofanyika katika ofisi za Wizara ya Maliasili nchini China
ambapo Mhe. Kairuki alishiriki kongamano la uwekezaji lililofanyika
nchini humo na kuibua fursa mbalimbali zilizopo katika sekta ya madini.
No comments :
Post a Comment