Na Alex Sonna,Dodoma
BUNGE limeelezwa kuwa mkoani Mara kuna mwalimu ambaye amewafanya kama wake zake watoto 10 wa darasa la kwanza.
Mbunge
wa Malindi, Ally Salehe (CUF), alitoa kauli hiyo wakati akiuliza swali
bungeni
ambapo amedai kwamba kuna tatizo la ubakaji limezidi kuwa kubwa
nchini.
Amefafanua
kuwa tatizo la ubakaji wa watoto linaonekana ni kubwa hapa nchini, tume
ya Katiba na sheria hivi karibuni walienda Mara na wakapata taarifa za
kutosha kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Mara Adam Malima kuhusiana na mwalimu
huyo.
“Kuna
mwalimu amewafanya wake zake watoto 10 wa darasa kwanza na kuna taarifa
nyingi za vitisho juu ya ubakaji kwa watu wazima na watoto,”amesema.
Mbunge
huyo akataka kujua kama Serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia na Wazee pamoja na Bunge haioni haja ya kuunda Tume ya
kutafuta utaratibu wa kwenda kulishughulikia jambo hili.
Amesema
tatizo ni kubwa na ukubwa wake unafikia mpaka watu wanauliwa na wengine
wanakimbilia upande wapili wa Kenya, Serikali ifikirie juu ya jambo
hilo kwa undani.
Baada
ya swali hilo, Spika wa Bunge, Jon Ndugai akachombeza kwa kumwambia
Mbunge wa Tarime Mjini, Ester Matiko kwamba sio wanaongoza kwa mambo
mengine tu kumbe na hayo.
Akijibu
swali hilo,kwa niaba, Waziri wa Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo,
Dk.Harisson Mwakyembe amesema jambo hilo ni baya na linatakiwa
litafutiwe ufumbuzi.
“Moja
ya shinikizo kubwa katika Nchi za Magharibi ni shinikizo la ndoa za
jinsia moja shinikizo la ushoga kama haki za kibinadamu….
“Bado
Nchi 38 kati ya 54 za Afrika zinapinga mambo hayo na Tanzania ikiwepo
yaani vitendo hivyo ni vya jinai na mtu anafungwa,”amesema.
Mwakyembe ameeleza kuwa changamoto katika jamii ni ndugu kuwaficha mashahidi hali ambayo imekuwa ikiwapa wakati mgumu.
“Tatizo
kubwa ni kwamba jamii inaficha haya matatizo mfano matatizo ya watoto
kulawitiwa yanafanyika sehemu kubwa na ndugu katika jamii na tukianza
upelelezi familia zina walinda wale wanaotakiwa kutoa ushahidi.
Amesema katika sheria kama hakuna ushahidi huwezi ukamfunga mtu kwahiyo sasa hivi ni kosa kubwa na adhabu ni kali.
Ametoa
wito kwa watanzania kutoa ushirikiano kwa vyombo vya dola ili tuweze
kuwapa hao wahalifu wanaojaribu kuchafua kizazi cha kesho.
No comments :
Post a Comment