NA MWAMVUA MWINYI, KIBAHA
JESHI la polisi
mkoani Pwani linamshikilia Robison Enerst (33) fundi ujenzi kwa kosa la
kumnyonga shingo, mwanae Modesta Robison mwezi umri wa miezi sita,
akidai sio mtoto wake.
Kamanda wa polisi
mkoani hapo, ACP Wankyo Nyigesa, alieleza kwamba,tukio hilo limetokea
april mosi, mwaka huu huko mtaa wa Vitendo kata ya Misugusugu ,Kibaha.
“Kabla ya kuolewa na
mtuhumiwa, mama wa mtoto (marehemu) alikuwa na mahusiano ya kimapenzi
na mwanaume mwingine ambae mtuhumiwa anamtuhumu ndio baba halali wa
mtoto “
“Hali hiyo ilisababisha migogoro ya mara kwa mara kati ya wazazi hao “alifafanua Wankyo.
Wankyo alibainisha,
wamemkamata mtuhumiwa ili aweze kuchukuliwa hatua za kisheria na mwili
wa marehemu umehifadhiwa hospital ya rufaa ya mkoa ya Tumbi, kabla ya
kukabidhiwa ndugu kwa mazishi.
Kamanda huyo alitoa
rai kwa wananchi, kuwa wanapokuwa na mashaka na jambo fulani la kihalifu
watoe taarifa mapema katika vituo vya polisi ili yaweze kushughulikiwa
mara moja kabla ya kuleta madhara yeyote kwa lengo la kudhibiti
watuhumiwa.
Hata hivyo, baada ya
kumhoji mama wa marehemu yeye alidai mtuhumiwa alishafanya majaribio ya
mtuhumiwa kumuua marehemu mwanae mara mbili.
Anaeleza, mara ya kwanza alitaka kumpa sumu ya vidonge lakini mama huyo aliwahi kumuokoa .
“Mara ya pili
mtuhumiwa alinoa panga ili amkate mtoto lakini hakufanikiwa pia kufikia
april 1, ambapo alimuua mtoto kwa kumnyonga shingo hadi kufariki dunia “
No comments :
Post a Comment