Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,
Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi) Selemani Jafo,akizungumza
na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo jijini Dodoma .
…………………..
Na.Alex Sonna,Dodoma
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,
Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi) Selemani Jafo,amesema
kuwa Serikali imewapa fursa wanafunzi waliofaulu kujiunga na kidato cha
tano kubadili tahsusi na kuchagua wanachokitaka kukisomea.
Hayo ameyasema hayo leo wakati
akitoa taarifa hiyo ya wanafunzi waliofaulu kujiunga na
kidato cha tano
kwa waandishi wa habari jijini Dodoma
Waziri Jafo amesema kuwa hali
hiyo inatokana na baadhi ya wanafunzi ambao hawakujaza vizuri tahasusi
zao kutokana na kutokuwa na uhakika wa ufaulu.
Jafo amesema ofisi yake haitatoa fursa ya mwanafunzi yeyote kubadili tahasusi anayotaka kama asipotumia fursa hiyo.
No comments :
Post a Comment