Pages

Friday, March 29, 2019

WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KIDATO CHA TANO WAPEWA FURSA KUBADILI TAHSUSI


JAFOO
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi) Selemani Jafo,akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo jijini Dodoma .
…………………..
Na.Alex Sonna,Dodoma
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi) Selemani Jafo,amesema kuwa Serikali imewapa fursa wanafunzi waliofaulu kujiunga na kidato cha tano kubadili tahsusi na kuchagua wanachokitaka kukisomea.
Hayo ameyasema hayo leo wakati  akitoa taarifa hiyo ya wanafunzi waliofaulu kujiunga na
kidato cha tano kwa waandishi wa habari jijini Dodoma
Waziri Jafo amesema kuwa  hali hiyo inatokana na baadhi ya wanafunzi ambao hawakujaza vizuri tahasusi zao kutokana na kutokuwa na uhakika wa ufaulu.
Jafo amesema ofisi yake haitatoa fursa ya mwanafunzi yeyote kubadili tahasusi anayotaka kama asipotumia fursa hiyo.

No comments:

Post a Comment