Friday, March 29, 2019

Video:Umuhimu wa fao la uzazi ZSSF kwa kinga ya ujauzito


http://www.ent-redefined.org/wp-content/uploads/2017/05/wp-1495827300988.jpgBaadhi ya akina mama wanachama wa mifuko ya hifadhi ya jamii wakifurahia kujifungua salama pamoja na watoto wao.


Na Christian Gaya: Majira Ijumaa, 29 Machi 2019
Kinga ya uzazi kwa akina mama lazima ichangie afya na ustawi wa mama pamoja na watoto wao ili kutimiza malengo ya namba 4 na 5 ya maendeleo ya millennia ya Tanzania kama mwanachama wa Umoja wa Mataifa.
Kutokana na kanuni na haki za uzazi na utaratibu wa Shirika la Kazi duniani (ILO) lengo la kubwa la kuwa na fao la uzazi ni...
kuhakikisha kuwa kazi za wanamke haziingiliwi na hali hatarishi ya afya ya wanamke pamoja na mtoto wake na kwamba shughuli za kujifungua hazikwamishi shughuli zao za kiuchumi za kila siku pamoja na usalama wa kazi zao iwe ya kujiajiri au kuajiriwa.
Utafiti pia unaonesha ya kuwa idadi kubwa ya akina mama wanaokufa kwa sababu ya kukosa huduma wakati wa kujifungua inaongezeka kila siku hasa kwa nchi zinazoendelea kama vile Tanzania.
Nchi zenye mapato ya chini kama Tanzania ambazo zina idadi kubwa ya vifo vya wajawazito na watoto vimekuwa vikitofautiana sana, na ni nchi 23 tu ambazo ziko kwenye kundi la kufikisha asilimia 75 katika kupunguza vifo vya wajawazito na watoto kufikia mwaka 2015.
Kwa mara ya kwanza katika karne, nguvu zaidi zimekuwa zikielekezwa kwenye lengo la millennia ya maendeleo namba 5, ambapo vifo vya wanawake wenye mimba na watoto vimeweza kupungua mpaka kufikia asilimia 35.
Kinga ya uzazi kwa  mwanamke ambaye ni mjamzito kabla ya kujifungua na baada ya kujifungua vile vile ni muhimu kuhakikisha ya kuwa mwanamke mzazi anapewa fursa sawa na matibabu katika sehemu za kazi ili kuhamasisha usawa wa jinsia na madaraka kwa wanawake.
Wanawake wengi wanakosa fursa ya kupatiwa malipo ya uzazi kabla ya kujifungua na hata baada ya kujifungua. Na wanawake wengi zaidi wanatishiwa kufukuzwa kazi  na hata kubaguliwa eti kwa sababu ni mjamzito au atakuja apate mimba.
Na inasekama pia ya kuwa karibu asilimia tisini na tisa ya wamama duniani wanaopoteza maisha yao wakati wa kujifungua hutokea Afrika na Tanzania ikiwa mojawapo, ingawa virusi vya ukimwi vikiwa mojawapo vinavyosababisha vifo vingi miongoni mwa wanawake wanategemea kujifungua au waliojifungua tayari. Na watoto wengi huzaliwa wakiwa wemekufa au mara tu mama kujifungua.
Na kwamba kati ya wajawazito kumi wanajifungua akina mama wanne hupoteza maisha pamoja na watoto wao. Na matukio haya yote hutokea nchi za Kiafrika ikiwemo Tanzania
Takwimu za hivi karibuni hapa nchini zinaonesha kwamba kwa mwaka, Tanzania inapoteza kina mama 7,900 kutokana na sababu zitokanazo na ujauzito. Idadi hiyo ni sawa na vifo 22 kwa siku. Magonjwa yanayoongoza kusababisha vifo vya wazazi nchini na mataifa mengine ni kifafa cha mimba, uzazi pingamizi, kupoteza damu nyingi wakati na baada ya kujifungua na maambukizi baada ya kujifungua.
Lakini pamoja na hayo mazingira ya kazi, biolojia na kifizikia na kemia mbalimbali za madawa zinazosaidia kuzalishia kazi zinaweza kuleta hali hatarishi zaidi kwa upande wa uzazi na watoto wanaozaliwa hasa kwa kukosa mikakati ya uhamasishaji wa elimu ya umma, miongozo na thathimini juu ya kinga ya mama anategemewa kujifungua au aliyetoka kujifungua.
Wanawake wengi ni wanachama wa mifuko ya hifadhi ya jamii lakini kwa sababu ya kukosa elimu juu ya mafao yanayotolewa na mifuko hii wanakosa huduma hizi za kinga ya uzazi. Na tunaona mara nyingi idadi kubwa ya akina mama kufa kabla au mara tu ya kujifungua. Hivyo hizi mimba nyingi zimekuwa zikitishia wamama na mara nyingi hufa mama au mtoto kama siyo wote.
Na elementi kuu za kinga za uzazi ni kama kupata likizo ya uzazi, kupata mafao taslimu ya kuhakikisha kuwa mama anaweza kujikimu yeye pamoja na mtoto wake wakati akiwa wa likizo ya uzazi, kuhakikisha kuwa anapatiwa matibabu, mama mjamzito anapatiwa kinga ya afya ya ujauzito bila kumsahau mtoto wake kupatiwa kinga kutokana na hali hatarishi zinazoweza kusababishwa na sehemu za kazi zenyewe.
Na ndiyo maana Mfuko wa hifadhi ya jamii Zanzibar yaani ZSSF unatoa fao hili la uzazi ambalo ni matokeo ya juhudi za Serikali za kupambana na kupunguza vifo vya wanawake wajawazito na watoto nchini.
Mfuko wa ZSSF unakwenda sambamba na malengo ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ambapo katika mwaka 2012 serikari ilitangaza rasmi kufuta malipo kwa wajawazito wakati wanapojifungua katika hospitali zote Unguja na Pemba
"Uamuzi huu wa kutoa fao na uzazi unakwenda sambamba na jitihada zinazoendelea kuchukuliwa na Serikali za kuimarisha ustawi wa kinamama wajawazito pamoja na kupunguza vifo vya watoto, ambavyo baadhi ya wakati husababishwa na umasikini unaopelekea watoto wakiwa tumboni kukosa mahitaji ya msingi kwa afya zao au huduma muhimu wakati wanapozaliwa na mara baada ya kuzaliwa,” Mkurugenzi Mwendeshaji wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar (ZSSF) Sabra Issa Machano anafafanua zaidi.   
Mkurugenzi Mwendeshaji anasema mafao ya uzazi yanalipwa kwa wanachama wanawake waliotimiza vigezo vya kuchangia kwa muda wa miezi 36, miezi sita iwe mfululizo kutoka tarehe anayoomba mafao, uthibitisho wa madaktari wenye kutambulika, vielelezo vya ushahidi wa kuthibitisha madai ya mafao, awe mjamzito ambaye ujauzito wake umefikia miezi 28, na awe amejifungua mtoto aliye hai.  
Na kigezo cha malipo hayo ya fao la uzazi ni asilimia 30 ya wastani wa mshahara wa mwezi wa wanachama wote wa Mfuko.
Machano anataja faida zake za fao la uzazi ya kwamba huziba pengo la akina mama wanaojifungua, husaidia huduma za matibabu za akina mama na watoto, husaidia gharama za matunzo na mahitaji ya mtoto, hulipwa fedha taslim, ni ya kipekee nchini ambapo malipo huongezeka ambapo mwanachama amejifungua mapacha.
Mafao haya hulipwa kila baada ya miaka mitatu isipokua pale ambapo mtoto amefariki wakati alipozaliwa au kabla ya kupita miaka hiyo mitatu. Mama mwanachama anatakiwa kuwasilisha   madai ndani ya siku 90 baada ya kujifungua.

No comments :

Post a Comment