Baadhi ya akina mama wanachama wa mifuko ya hifadhi ya jamii
wakifurahia kujifungua salama pamoja na watoto wao.
Na Christian Gaya: Majira Ijumaa, 29 Machi 2019
Kinga
ya uzazi kwa akina mama lazima ichangie afya na ustawi wa mama pamoja na watoto
wao ili kutimiza malengo ya namba 4 na 5 ya maendeleo ya millennia ya Tanzania
kama mwanachama wa Umoja wa Mataifa.
Kutokana
na kanuni na haki za uzazi na utaratibu wa Shirika la Kazi duniani (ILO) lengo
la kubwa la kuwa na fao la uzazi ni...
kuhakikisha kuwa kazi za wanamke haziingiliwi
na hali hatarishi ya afya ya wanamke pamoja na mtoto wake na kwamba shughuli za
kujifungua hazikwamishi shughuli zao za kiuchumi za kila siku pamoja na usalama
wa kazi zao iwe ya kujiajiri au kuajiriwa.
Utafiti
pia unaonesha ya kuwa idadi kubwa ya akina mama wanaokufa kwa sababu ya kukosa
huduma wakati wa kujifungua inaongezeka kila siku hasa kwa nchi zinazoendelea
kama vile Tanzania.
Nchi zenye mapato ya
chini kama Tanzania ambazo zina idadi kubwa ya vifo vya wajawazito na watoto
vimekuwa vikitofautiana sana, na ni nchi 23 tu ambazo ziko kwenye kundi la
kufikisha asilimia 75 katika kupunguza vifo vya wajawazito na watoto kufikia
mwaka 2015.
Kwa mara ya kwanza
katika karne, nguvu zaidi zimekuwa zikielekezwa kwenye lengo la millennia ya
maendeleo namba 5, ambapo vifo vya wanawake wenye mimba na watoto vimeweza
kupungua mpaka kufikia asilimia 35.
Kinga
ya uzazi kwa mwanamke ambaye ni mjamzito
kabla ya kujifungua na baada ya kujifungua vile vile ni muhimu kuhakikisha ya
kuwa mwanamke mzazi anapewa fursa sawa na matibabu katika sehemu za kazi ili
kuhamasisha usawa wa jinsia na madaraka kwa wanawake.
Wanawake
wengi wanakosa fursa ya kupatiwa malipo ya uzazi kabla ya kujifungua na hata
baada ya kujifungua. Na wanawake wengi zaidi wanatishiwa kufukuzwa kazi na hata kubaguliwa eti kwa sababu ni mjamzito
au atakuja apate mimba.
Na inasekama pia ya kuwa karibu asilimia tisini na tisa ya
wamama duniani wanaopoteza maisha yao wakati wa kujifungua hutokea Afrika na
Tanzania ikiwa mojawapo, ingawa
virusi vya ukimwi vikiwa mojawapo vinavyosababisha vifo vingi miongoni mwa
wanawake wanategemea kujifungua au waliojifungua tayari. Na watoto wengi huzaliwa wakiwa wemekufa au mara tu mama
kujifungua.
Na
kwamba kati ya wajawazito kumi wanajifungua akina mama wanne hupoteza maisha
pamoja na watoto wao. Na matukio haya yote hutokea nchi za Kiafrika ikiwemo
Tanzania
Takwimu
za hivi karibuni hapa nchini zinaonesha kwamba kwa mwaka, Tanzania inapoteza
kina mama 7,900 kutokana na sababu zitokanazo na ujauzito. Idadi hiyo ni sawa
na vifo 22 kwa siku. Magonjwa yanayoongoza kusababisha vifo vya wazazi nchini
na mataifa mengine ni kifafa cha mimba, uzazi pingamizi, kupoteza damu nyingi
wakati na baada ya kujifungua na maambukizi baada ya kujifungua.
Lakini
pamoja na hayo mazingira ya kazi, biolojia na kifizikia na kemia mbalimbali za
madawa zinazosaidia kuzalishia kazi zinaweza kuleta hali hatarishi zaidi kwa
upande wa uzazi na watoto wanaozaliwa hasa kwa kukosa mikakati ya uhamasishaji
wa elimu ya umma, miongozo na thathimini juu ya kinga ya mama anategemewa kujifungua
au aliyetoka kujifungua.
Wanawake wengi ni wanachama wa mifuko ya hifadhi ya jamii
lakini kwa sababu ya kukosa elimu juu ya mafao yanayotolewa na mifuko hii
wanakosa huduma hizi za kinga ya uzazi. Na tunaona mara nyingi idadi kubwa ya akina
mama kufa kabla au mara tu ya kujifungua. Hivyo hizi mimba nyingi zimekuwa
zikitishia wamama na mara nyingi hufa mama au mtoto kama siyo wote.
Na
elementi kuu za kinga za uzazi ni kama kupata likizo ya uzazi, kupata mafao
taslimu ya kuhakikisha kuwa mama anaweza kujikimu yeye pamoja na mtoto wake
wakati akiwa wa likizo ya uzazi, kuhakikisha kuwa anapatiwa matibabu, mama
mjamzito anapatiwa kinga ya afya ya ujauzito bila kumsahau mtoto wake kupatiwa
kinga kutokana na hali hatarishi zinazoweza kusababishwa na sehemu za kazi
zenyewe.
Na
ndiyo maana Mfuko wa hifadhi ya jamii Zanzibar yaani ZSSF unatoa fao hili la
uzazi ambalo ni matokeo ya juhudi za Serikali za kupambana na kupunguza vifo
vya wanawake wajawazito na watoto nchini.
Mfuko
wa ZSSF unakwenda sambamba na malengo ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar
ambapo katika mwaka 2012 serikari ilitangaza rasmi kufuta malipo kwa wajawazito
wakati wanapojifungua katika hospitali zote Unguja na Pemba
"Uamuzi huu wa kutoa fao na uzazi unakwenda sambamba
na jitihada zinazoendelea kuchukuliwa na Serikali za kuimarisha ustawi wa
kinamama wajawazito pamoja na kupunguza vifo vya watoto, ambavyo baadhi ya
wakati husababishwa na umasikini unaopelekea watoto wakiwa tumboni kukosa
mahitaji ya msingi kwa afya zao au huduma muhimu wakati wanapozaliwa na mara baada
ya kuzaliwa,” Mkurugenzi
Mwendeshaji wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar (ZSSF) Sabra Issa Machano
anafafanua zaidi.
Mkurugenzi
Mwendeshaji anasema
mafao ya uzazi yanalipwa kwa wanachama wanawake waliotimiza vigezo vya kuchangia
kwa muda wa miezi 36, miezi sita iwe mfululizo kutoka tarehe anayoomba mafao,
uthibitisho wa madaktari wenye kutambulika, vielelezo vya ushahidi wa
kuthibitisha madai ya mafao, awe mjamzito ambaye ujauzito wake umefikia miezi
28, na awe amejifungua mtoto aliye hai.
Na kigezo cha malipo hayo ya fao la uzazi ni asilimia 30 ya wastani wa
mshahara wa mwezi wa wanachama wote wa Mfuko.
Machano anataja
faida zake za fao la uzazi ya kwamba huziba pengo la akina mama wanaojifungua, husaidia huduma
za matibabu za akina mama na watoto, husaidia gharama za matunzo na mahitaji ya
mtoto, hulipwa fedha taslim, ni ya kipekee nchini ambapo malipo huongezeka
ambapo mwanachama amejifungua mapacha.
Mafao haya hulipwa kila baada ya miaka mitatu isipokua pale ambapo
mtoto amefariki wakati alipozaliwa au kabla ya kupita miaka hiyo mitatu. Mama mwanachama
anatakiwa kuwasilisha madai ndani ya siku 90 baada ya kujifungua.
No comments:
Post a Comment