Friday, March 29, 2019

TEHAMA KUSAIDIA SEKTA YA AFYA AFRIKA MASHARIKI


IMG-20190329-WA0041
Waziri wa Afya, maendeleo ya jamii, jinsia na watoto Ummy Mwalimu akiongea na waandishi wa habari katika mkutano ambao umewakutanisha wadau wa Afya kutoka katika jumuiya ya Afrika Mashariki
…………………….
NA EMMANUEL MBATILO
Nchi za Afrika MasharikI zimekubaliana kwa pamoja kutumia huduma za Tehama katika kutoka huduma za afya ili kuimarisha upatikanaji wa huduma za kimatibabu katika nchi hizo.
Akizungumza katika kufunga  Mkutano wa siku tatu wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki ambao ulikuwa unahusu maswala ya afya na sayansi Waziri wa Afya, maendeleo ya jamii jinsia wazee na wazee mhe Ummy Mwalimu, amesema  mambo makubwa matatu ambayo yamejitokeza katika mkutano huo ni pamoja na kukubaliana kwa pamoja kama nchi hizo ni  kuongeza uekezaji na matumizi ya tehama katika kuboresha utoaji wa huduma za afya.
“Katika eneo la kuongeza matumizi ya tehema yamebainika maeneo matatu ambayo tunaweza kupata matokeo ya haraka, eneo la kwanza ni kutumia tehama katika kudhibiti magonjwa  na wengi wameniuliza kuhusu homa ya dengu, watu wanaumwa sana sasa hizi taarifa tutakuwa tunazikusanya kutoka katika vituo vinavyotoa huduma za afya ndani ya nchi vitakuwa vinakuja moja kwa moja wizarani kwahiyo tumeona eneo hili tukiboresha vizuri katika ukusanyaji wa taarifa katika udhibiti wagonjwa litatusaidia sana’’. Amesema ummy.
Aidha Ummy ameongeza kuwa katika eneo la pili wamejadili  na kukubaliana kutumia Tehama katika kutoa huduma za matibabu ya kibingwa kwa kuwa  kuna uhaba wa watumishi wa afya hasa wataalamu.
Kwa upande wa mganga mkuu wa serikali Mohammed Kambi amesema kuwa katika vituo mahili ambavyo vipo katika jumuiya hiyo haviangalii hutoaji huduma pekee kuna hutoaji huduma, suala la utafiti na kuna suala ya mafunzo, hivyo havizuiii kutokua na ushirikiana na vituo vingine katika masuala yote ya huduma.
“Kama jumuiya tunaanzisha vituo vya kutolea huduma mahili za kibingwa kwa hapa Tanzania tutakuwa na kituo mahili kwa magonjwa ya moyo na mishipa ya damu, Kenya watakuwa na kituo mahili kwa mgonjwa ya ya figo, Uganda watkuwa na kituo mahili kwa matibabu ya magonjwa ya kansa na hivyo hivyo katika nchi nyingine za Afrika Mashariki”. Amesema Kambi.

No comments :

Post a Comment