Waziri wa Afya,
maendeleo ya jamii, jinsia na watoto Ummy Mwalimu akiongea na waandishi
wa habari katika mkutano ambao umewakutanisha wadau wa Afya kutoka
katika jumuiya ya Afrika Mashariki
…………………….
NA EMMANUEL MBATILO
Nchi za Afrika
MasharikI zimekubaliana kwa pamoja kutumia huduma za Tehama katika
kutoka huduma za afya ili kuimarisha upatikanaji wa huduma za kimatibabu
katika nchi hizo.
Akizungumza katika
kufunga Mkutano wa siku tatu wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki
ambao ulikuwa unahusu maswala ya afya na sayansi Waziri wa Afya,
maendeleo ya jamii jinsia wazee na wazee mhe Ummy Mwalimu, amesema
mambo makubwa matatu ambayo yamejitokeza katika mkutano huo ni pamoja
na kukubaliana kwa pamoja kama nchi hizo ni kuongeza uekezaji na
matumizi ya tehama katika kuboresha utoaji wa huduma za afya.
“Katika eneo la
kuongeza matumizi ya tehema yamebainika maeneo matatu ambayo tunaweza
kupata matokeo ya haraka, eneo la kwanza ni kutumia tehama katika
kudhibiti magonjwa na wengi wameniuliza kuhusu homa ya dengu, watu
wanaumwa sana sasa hizi taarifa tutakuwa tunazikusanya kutoka katika
vituo vinavyotoa huduma za afya ndani ya nchi vitakuwa vinakuja moja kwa
moja wizarani kwahiyo tumeona eneo hili tukiboresha vizuri katika
ukusanyaji wa taarifa katika udhibiti wagonjwa litatusaidia sana’’.
Amesema ummy.
Aidha Ummy ameongeza
kuwa katika eneo la pili wamejadili na kukubaliana kutumia Tehama
katika kutoa huduma za matibabu ya kibingwa kwa kuwa kuna uhaba wa
watumishi wa afya hasa wataalamu.
Kwa upande wa mganga
mkuu wa serikali Mohammed Kambi amesema kuwa katika vituo mahili ambavyo
vipo katika jumuiya hiyo haviangalii hutoaji huduma pekee kuna hutoaji
huduma, suala la utafiti na kuna suala ya mafunzo, hivyo havizuiii
kutokua na ushirikiana na vituo vingine katika masuala yote ya huduma.
“Kama jumuiya
tunaanzisha vituo vya kutolea huduma mahili za kibingwa kwa hapa
Tanzania tutakuwa na kituo mahili kwa magonjwa ya moyo na mishipa ya
damu, Kenya watakuwa na kituo mahili kwa mgonjwa ya ya figo, Uganda
watkuwa na kituo mahili kwa matibabu ya magonjwa ya kansa na hivyo hivyo
katika nchi nyingine za Afrika Mashariki”. Amesema Kambi.
No comments:
Post a Comment