Waziri wa Maji, Mhe. Profesa
Makame Mbarawa (Mb) akiwasili ofisini kwa Mkuu wa Mkoa wa Songwe
Brigedia Generali Mstaafu Nicodemus Mwangela katikati ni Katibu Tawala
wa Mkoa wa Songwe David Kafulila.
Waziri wa Maji, Mhe. Profesa
Makame Mbarawa (Mb) akisaini kitabu cha wageni ofisini kwa Mkuu wa Mkoa
wa Songwe Brigedia Generali Mstaafu Nicodemus Mwangela.
Waziri wa Maji, Mhe. Profesa
Makame Mbarawa (Mb) akipata maelezo ya ujenzi wa tanki (halipo pichani)
kutoka kwa Mhandisi wa Maji wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira
Mbeya Mhandisi Ndele Mengo. Kushoto kwa Waziri ni Mkuu wa Wilaya ya
Momba Halmashauri ya Tunduma Bw. Juma Said Irando.
Moja ya miundombinu ya maji inayojengwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Ileje ambapo Waziri Mbarawa alifika kukagua ujenzi huo.
…………………………
Waziri wa Maji, Mhe. Profesa
Makame Mbarawa (Mb) leo ameanza ziara ya kukagua miradi ya maji mkoani
Songwe hususan miradi yenye changamoto ambayo imechukua
muda mrefu
kukamilika.
Waziri aliyasema hayo alipofika
ofisini kwa Mkuu wa Mkoa wa Songwe Brigedia Jenerali Nicodemas Mwangela
mara tu baada ya kuwasili ofisini kwa Mkuu wa mkoa huyo.
“Nimekuja kukagua miradi ambayo
ina changamoto kubwa ambayo haijakamilika kwa muda mrefu na wananchi
wanaisubiri kwa muda mrefu” alisema Profesa Makame Mbarawa.
Serikali kupitia Ilani ya Chama
cha Mapinduzi imeahidi kwamba ifikapo mwaka 2020 kwenye miji mikuu ya
mikoa wananchi wawe wamepata maji asilimia 95 na miji ya wilaya asilimia
90 na vijijini asilimia 85.
Hata hivyo, Waziri alisisitiza
kwamba tunapopewa dhamana ya kusimamia miradi ya maji inabidi lazima
tusimamie kwa uadilifu, ukaribu zaidi na kuhakikisha kwamba wakandarasi
wanaolipwa pesa kwa ajili ya kukamilisha miradi ya maji wanaanza kazi
mara moja baada ya kulipwa, kwa sababu wakandarasi wengine wamekuwa na
tabia ya kuchukua pesa za miradi ya maji na kupeleka kwenye miradi
mingine.
Naye, Mhandisi wa Majisafi na
Usafi wa Mazingira Mbeya, Mhandisi Ndele Mengo akitoa taarifa ya
utekelezaji wa Mradi wa Itumba Isongole amesema Mradi huo unatekelezwa
na Mkandarasi Singilimo Enterprises Ltd. ya jijini Dar es Salaam ambapo
gharama ya mradi ni Tsh. 804,162,330/= na hadi sasa ameshalipwa Tsh.
313,238,780/= ambazo zikihusisha uchimbaji wa mitaro kwenye bomba kuu
chanzo cha umbali wa mita 4332 na ulazaji wa bomba za plastic wenye
kipenyo cha nchi 8 umbali wa mita 3924 pamoja na tanki la kuhifadhia
maji lenye ujazo wa lita laki. Mradi huu amesema unasimamiwa na Mamlaka
ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Mbeya. Matazamio ya kukamilika kwa
mradi huu ni 30/5/2019.
Aidha, Waziri Profesa Mbarawa
ameagiza mradi wa Itumba Isongole uwe umekamilika ifikapo tarehe
30/5/2019 na mradi wa maji wa mji wa Tunduma uwe umekamilika ifikapo
13/4/2019 ili wananchi wapate majisafi na salama kwa sababu karibu
wakandarasi wote wameshalipwa pesa zao walizokuwa wanaidai Serikali.
No comments:
Post a Comment