Mkurugenzi
Mtendaji wa Wakala wa Mafunzo kwa Njia ya Mtandao (TaGLA), Bw. Charles
Senkondo akielezea majukumu ya ofisi yake kwa Naibu Waziri, Ofisi ya
Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary
Mwanjelwa (Mb) alipofanya ziara ya kikazi katika ofisi hiyo jijini Dar
es Salaam kwa lengo la kuhimiza uwajibikaji.
Naibu Waziri,
Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.
Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) na Mkurugenzi Mtendaji wa Wakala wa Mafunzo kwa
Njia ya Mtandao (TaGLA), Bw. Charles Senkondo wakishuhudia teknolojia
ya mawasiliano kwa njia ya video kwa kuunganishwa na Chuo cha Utumishi
wa Umma Nairobi, Kenya, alipofanya ziara ya kikazi katika ofisi hiyo
jijini Dar es Salaam kwa lengo la kuhimiza uwajibikaji.
Naibu Waziri,
Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.
Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb), Mkurugenzi Mtendaji wa Wakala wa Mafunzo kwa
Njia ya Mtandao (TaGLA), Bw. Charles Senkondo na watumishi wa TaGLA
wakishuhudia teknolojia ya mawasiliano kwa njia ya video kwa
kuunganishwa na Chuo cha Utumishi wa Umma Nairobi, Kenya.
Meneja TEHAMA wa
Wakala wa Mafunzo kwa Njia ya Mtandao (TaGLA), Bw. Emmanuel Tessua
akitoa ufafanuzi jinsi teknolojia inavyofanya kazi katika wakala huo kwa
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala
Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb), alipofanya ziara ya kikazi katika
ofisi hiyo jijini Dar es Salaam kwa lengo la kuhimiza uwajibikaji.
Naibu Waziri,
Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.
Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akipokea zawadi kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji
wa Wakala wa Mafunzo kwa Njia ya Mtandao (TaGLA), Bw. Charles Senkondo
alipofanya ziara ya kikazi katika ofisi hiyo jijini Dar es Salaam kwa
lengo la kuhimiza uwajibikaji.
……………………
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais,
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary
Mwanjelwa (Mb) amewataka watumishi wa Wakala wa Mafunzo kwa Njia ya
Mtandao (TaGLA) kutumia taaluma yao kubuni mbinu mbalimbali
zitakazovutia taasisi za umma, sekta binafsi na watanzania kwa ujumla
kupenda kutumia mifumo ya TEHAMA ili kuiongezea
Serikali mapato na
kupunguza gharama.
“Mkiwa kama wataalam wa masuala ya
mawasiliano kwa njia ya video na mafunzo kwa njia ya mtandao, jaribuni
kusumbua akili zenu kwa kuweka njia madhubuti zitakazowavutia watanzania
kupenda wenyewe kutumia mawasiliano kwa njia ya video na mafunzo kwa
njia ya mtandao ili kuendana na teknolojia na kupunguza gharama,” Mhe.
Dkt. Mwanjelwa amesisitiza.
Akizungumza na watumishi wa Wakala
wa Mafunzo kwa Njia ya Mtandao (TaGLA) alipofanya ziara ya kikazi
katika wakala huo, Mhe. Mwanjelwa amesema ni lazima watumishi wa Wakala
huo wafanye kazi zenye matokea chanya ambazo zitapunguza gharama kwa
serikali kama ambavyo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt.
John Magufuli anasisitza.
“Ni lazima tujue kiongozi wetu
Mkuu wa Nchi anataka nini katika utendaji kazi wetu, tufanye kazi kwa
bidii na kuipunguzia serikali gharama zisizokuwa za lazima,” Mhe. Dkt.
Mwanjelwa ameongeza.
Aidha, amewapongeza watumishi wa
wakala huo kwa kazi nzuri wanayoifanya na kuwataka kuangalia namna bora
ya kujitangaza ili kufahamika na kupata wateja wengi watakaotumia
mawasiliano kwa njia ya video na mafunzo kwa njia ya mtandao ili
kuiongezea serikali mapato.
Aidha, ameahidi kutoa ushirikiano
kwa watumishi wa wakala huo katika kutekeleza majukumu yake na kuboresha
utuoaji huduma kwa umma.
Katika ziara hiyo, Mhe. Mwanjelwa
ameshuhudia teknolojia ya mawasiliano kwa njia ya video kwa kuunganishwa
na Chuo cha Utumishi wa Umma Nairobi, Kenya na ofisi yake jijini
Dodoma.
No comments :
Post a Comment