Pages

Friday, March 29, 2019

MHE. MWANJELWA AWATAKA WATUMISHI WA TaGLA KUWA WABUNIFU ILI KUWAVUTIA WATANZANIA KUPENDA KUTUMIA MAWASILIANO KWA NJIA YA VIDEO NA KUIPUNGUZIA SERIKALI GHARAMA


IMG_2631
Mkurugenzi Mtendaji wa Wakala wa Mafunzo kwa Njia ya Mtandao (TaGLA), Bw. Charles Senkondo akielezea majukumu ya ofisi yake kwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) alipofanya ziara ya kikazi katika ofisi hiyo jijini Dar es Salaam kwa lengo la kuhimiza uwajibikaji.
IMG_2655
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) na Mkurugenzi Mtendaji wa Wakala wa Mafunzo kwa Njia ya Mtandao (TaGLA), Bw. Charles Senkondo   wakishuhudia teknolojia ya mawasiliano kwa njia ya video kwa kuunganishwa na Chuo cha Utumishi wa Umma Nairobi, Kenya, alipofanya ziara ya kikazi katika ofisi hiyo jijini Dar es Salaam kwa lengo la kuhimiza uwajibikaji.
IMG_2666
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb), Mkurugenzi Mtendaji wa Wakala wa Mafunzo kwa Njia ya Mtandao (TaGLA), Bw. Charles Senkondo na watumishi wa TaGLA wakishuhudia teknolojia ya mawasiliano kwa njia ya video kwa kuunganishwa na Chuo cha Utumishi wa Umma Nairobi, Kenya.
IMG_2710
Meneja TEHAMA wa Wakala wa Mafunzo kwa Njia ya Mtandao (TaGLA), Bw. Emmanuel Tessua akitoa ufafanuzi jinsi teknolojia inavyofanya kazi katika wakala huo kwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb), alipofanya ziara ya kikazi katika ofisi hiyo jijini Dar es Salaam kwa lengo la kuhimiza uwajibikaji.
IMG_2825
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akipokea zawadi kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Wakala wa Mafunzo kwa Njia ya Mtandao (TaGLA), Bw. Charles Senkondo alipofanya ziara ya kikazi katika ofisi hiyo jijini Dar es Salaam kwa lengo la kuhimiza uwajibikaji.
……………………
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) amewataka watumishi wa Wakala wa Mafunzo kwa Njia ya Mtandao (TaGLA) kutumia taaluma yao kubuni mbinu mbalimbali zitakazovutia taasisi za umma, sekta binafsi na watanzania kwa ujumla kupenda kutumia mifumo ya TEHAMA ili kuiongezea
Serikali mapato na kupunguza gharama.
“Mkiwa kama wataalam wa masuala ya mawasiliano kwa njia ya video na mafunzo kwa njia ya mtandao, jaribuni kusumbua akili zenu kwa kuweka njia madhubuti zitakazowavutia watanzania kupenda wenyewe kutumia mawasiliano kwa njia ya video na mafunzo kwa njia ya mtandao ili kuendana na teknolojia na kupunguza gharama,” Mhe. Dkt. Mwanjelwa amesisitiza.
Akizungumza na watumishi wa Wakala wa Mafunzo kwa Njia ya Mtandao (TaGLA) alipofanya ziara ya kikazi katika wakala huo, Mhe. Mwanjelwa amesema ni lazima watumishi wa Wakala huo wafanye kazi zenye matokea chanya ambazo zitapunguza gharama kwa serikali kama ambavyo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Magufuli anasisitza.
“Ni lazima tujue kiongozi wetu Mkuu wa Nchi anataka nini katika utendaji kazi wetu, tufanye kazi kwa bidii na kuipunguzia serikali gharama zisizokuwa za lazima,” Mhe. Dkt. Mwanjelwa ameongeza.
Aidha, amewapongeza watumishi wa wakala huo kwa kazi nzuri wanayoifanya na kuwataka kuangalia namna bora ya kujitangaza ili kufahamika na kupata wateja wengi watakaotumia mawasiliano kwa njia ya video na mafunzo kwa njia ya mtandao ili kuiongezea serikali mapato.
Aidha, ameahidi kutoa ushirikiano kwa watumishi wa wakala huo katika kutekeleza majukumu yake na kuboresha utuoaji huduma kwa umma.
Katika ziara hiyo, Mhe. Mwanjelwa ameshuhudia teknolojia ya mawasiliano kwa njia ya video kwa kuunganishwa na Chuo cha Utumishi wa Umma Nairobi, Kenya na ofisi yake jijini Dodoma.

No comments:

Post a Comment