Na Mwandishi Maalum – JKCI
Jumla ya watu 62 wamefanywa vipimo vya kuangalia jinsi moyo unavyofanya kazi (Echo Cardiogram) na
umeme wa moyo (ECG) wakati wa punguzo la gharama za matibabu kwa
wagonjwa wa kulipia lililotolewa na Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete
(JKCI).
Punguzo hilo lilitolewa hivi karibuni na Taasisi hiyo ikiwa ni sehemu ya kusherehekea ushindi wa timu ya Taifa ya mpira wa miguu kwa kuifunga timu ya Uganda mabao 3-0 na kuweza
kushiriki katika mashindano ya Taifa Bingwa Barani Afrika AFCON. 2019.
Akiongea
na mwandishi wa habari hizi jijini Dar es Salaam Mkurugenzi wa
Kurugenzi ya Tiba Shirikishi ambaye pia ni daktari bingwa wa magonjwa ya
moyo Dkt. Delila Kimambo alisema kati ya wagonjwa 62 waliopima afya zao nane walikuwa ni watoto.
Dkt. Delila alisema katika kusherehekea ushindi wa timu ya Taifa Taasisi hiyo imeona ni vyema kufungua milango na kuwahamasisha wananchi kujitokeza kupima afya ya moyo.
“Kati ya watu 62 tuliowapima 19 tuliwakuta na matatizo ya moyo ambapo wa nne wanatakiwa kufanyiwa uchunguzi
wa mishipa ya damu ya moyo, mmoja kati yao ameshafanyiwa na kukutwa na
tatizo la kuziba kwa mishipa miwili ya damu ameshazibuliwa mshipa mmoja
na anaendelea vizuri”,.
“Wengine wanne walikutwa na tatizo la valvu ambapo wawili wanatakiwa kufanyiwa upasuaji wa kubadilisha valve. Wengine tumewakuta na shinikizo la juu la damu”,.
“Zoezi
hili limefanyika vizuri, tunafahamu kuwa kuna wananchi ambao huwa
wanahitaji vipimo vya moyo kwa dharula na hawawezi kufika kwetu kutokana
na shida mbalimbali za maisha, hivyo tulitoa punguzo hili la bei ili kuwafungulia milango ya kupata matibabu ya vipimo vinavyoweza kugundua kama mtu ana magonjwa ya moyo”, alisema Dkt. Delila.
Dkt. Delila alimalizia kwa kuwaomba watanzania kuwa na utamaduni wa kupenda kupima afya zao mara kwa mara ,kupata matibabu na majibu ya magonjwa yanayowasumbua kutoka kwa wataalamu wa magonjwa husika.
Kwa upande wake Frank Karia ambaye ni makazi wa Mwanza alisema alipewa Rufaa kutoka
hospitali ya rufaa ya Bugando na kufika JKCI siku ya Jumatatu ambapo
kulikuwa na punguzo la bei na kubahatika kufanyiwa vipimo vya ECHO na ECG baada ya kufanyiwa vipimo aligundulika kuziba kwa mishipa miwili inayopeleka damu kwenye moyo.
“Baada
ya kukutwa na tatizo ndani ya wiki moja tayari nimeshazibuliwa mshipa
mmoja wa damu na hali yangu inaendelea vizuri kama unavyoniona, baada ya
wiki mbili nitarudi kliniki . Leo tarehe 29/03/2019nimeruhusiwa kwenda
nyumbani, kwa kweli sikutegemea kama ningepata huduma hii kwa kipindi
cha wiki moja” alisema Karia.
Alisema huduma zinazotolewa na Taasisi hiyo ni za kimataifa na kuwaomba waendelee kutoa elimu kwa umma ili wananchi wafahamu zaidi huduma zinazotolewa.
No comments:
Post a Comment