Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini
Prof. Simon Msanjila (kulia) akizungumza jambo wakati wa kikao baina
yake na Viongozi wa Jumuiya ya Watendaji Wakuu wa Taasisi Binafsi.
Kushoto ni mmoja wa viongozi hao.
Mmoja wa Viongozi wa Jumuiya ya
Watendaji Wakuu wa Taasisi Binafsi akizungumza jambo katika kikao hicho.
Kulia ni Kamishna Msaidizi wa Wizara ya Madini, Godfrey Nyamrunda
Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini
Prof.Simon Msanjila akimsikiliza mmoja wa Viongozi wa Jumuiya ya
Watendaji Wakuu wa Taasisi Binafsi.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini
Prof. Simon Msanjila wakijadiliana jambo na baadhi Viongozi wa Jumuiya
ya Watendaji Wakuu wa Taasisi Binafsi.
Mmoja wa viongozi wa jumuiya
Jumuiya ya Watendaji Wakuu wa Taasisi Binafsi, Francis Nanai ambaye pia
ni Mkurugenzi Mtendajiwa Kampuni ya Mwananchi Communications Limited,
akizungumza jambo
Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini
Prof. Simon Msanjila katika picha ya pamoja na Viongozi wa Jumuiya ya
Watendaji Wakuu wa Taasisi Binafsi.
…………………
Na Asteria Muhozya, Dodoma
Serikali kupitia Wizara ya Madini
inakamilisha taratibu za utoaji wa Leseni kwa Migodi Mikubwa ambazo
hazijawahi kutolewa nchini, huku migodi hiyo ikitarajiwa kuanzishwa hivi
karibuni.Hayo yamebainishwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini Prof.
Simon Msanjila alipokutana na viongozi wa Jumuiya ya Watendaji Wakuu wa
Taasisi Binafsi ofisini kwake,
jijini Dodoma.Viongozi hao walikutana na
Prof. Msanjila Februari 26, kwa lengo la kujitambulisha, kuelewa
shughuli za serikali upande wa sekta ya madini, kupata uelewa kuhusu
mabadiliko ya Sheria ya Madini na namna pande hizo mbili zinavyoweza
kushirikiana katika kuendeleza sekta husika.Prof. Msanjila
aliwakaribisha viongozi hao kwenye sekta ya madini huku akiwataka
kuzishawishi kampuni mbalimbali kuwekeza nchini hususani katika shughuli
za uongezaji thamani madini na kueleza kuwa, suala hilo ni miongoni mwa
maeneo ambayo serikali inayapa kipaumbele ikiwemo ujenzi wa vinu vya
kusafisha na kuyeyusha madini. Akizungumzia Sheria Mpya ya Madini ya
Mwaka 2017, Prof. Msanjila amesema hakuna tatizo lolote katika
utekelezaji wa sheria na kueleza kuwa, serikali kupitia wizara ya madini
inapokea wawekezaji wengi wenye utayari na nia ya kuwekeza nchini huku
utekelezaji wa sheria hiyo ukiwa si kikwazo na kuongeza kwamba, “hakuna
mahali ambapo serikali inatengeneza sheria kwa ajili ya kumkandamiza
mfanya biashara”. “Hakuna tatizo lolote kwenye sheria ya madini. Hata
wageni huwa tunakaa nao tunawaelimisha na wanatuelewa vizuri. Kama kuna
dosari ni vitu ambavyo tunaweza kuvirekebisha na tayari
tumekwishakufanya hivyo kwa baadhi ya maeneo,” alisema Prof.
Msanjila.Aidha, katika kikao hicho Prof. Msanjila alitoa ushauri kwa
viongozi hao kujitangaza zaidi kuhusu kazi zao huku akiwataka kutafuta
wasaa kwa ajili ya pande hizo mbili kukutana ili wizara iweze kutoa
elimu zaidi kwa Jumuiya hiyo kuhusu sekta ya madini ikiwemo fursa za
uwekezaji zilizopo.Pia, Prof. Msanjila alisema kuwa suala la kuaminiana
linaweza kujengwa huku akiwataka watanzania kuwa wazalendo na namna
wanavyotumia fedha za umma. Prof.
Msanjila alizungumzia jambo hilo baada ya mmoja wa viongozi hao kueleza
kuwa, bado kuna hali ya kutokuaminiana baina ya serikali na taasisi
binafsi.Kwa upande wake, mmoja wa viongozi wa jumuiya hiyo, Francis
Nanai ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mwananchi
Communications Limited amemweleza Prof. Msanjila kuwa, kama viongozi wa
umoja huo, wamezipokea changamoto zilizotolewa kwao na Prof. Msanjila
ikiwemo ushauri wa kukutana na wizara kwa lengo la kupata ufafanuzi na
elimu zaidi kuhusu sekta ya madini.
No comments :
Post a Comment