Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya
Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akizungumza na wananchi kuhusu matukio
ya utekwaji na kuuliwa kwa watoto katika Mkoa wa Njombe, ambapo aliwaasa
wananchi kutoa ushirikiano kwa Jeshi la Polisi katika juhudi za
kukomesha matukio hayo.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
Mkuu wa Wilaya ya Njombe, Ruth
Msafiri akizungumza na wananchi kuhusu matukio ya utekwaji na kuuliwa
kwa watoto katika Mkoa wa Njombe, ambapo aliahidi kushirikiana na Vyombo
vya Ulinzi na Usalama kukomesha matukio ya utekaji na kuuliwa kwa
watoto.
Mkazi wa Njombe, Alex Msupilo
akimuuliza maswali Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi
Hamad Masauni(hayupo pichani), juu ya hatua zilizochukuliwa na Serikali
kukagua leseni za waganga wa tiba asilia ambao wamekua wakitajwa kufanya
tiba chonganishi zinazopelekea kutokea kwa matukio ya utekaji na
kuuliwa kwa watoto katika mkoa huo.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya
Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akizungumza katika kikao kidogo
kilichohusisha Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Njombe na baadhi
ya wananchi lengo ikiwa ni kujadili juu ya matukio ya utekaji na kuuliwa
kwa watoto mkoani hapo.
No comments :
Post a Comment