Pages

Wednesday, January 30, 2019

MASAUNI AZUNGUMZA NA WANANCHI WA NJOMBE KUHUSU UTEKWAJI NA MAUAJI YA WATOTO


 
PIX%2B1
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akizungumza na wananchi  kuhusu matukio ya utekwaji na kuuliwa kwa watoto katika Mkoa wa Njombe, ambapo aliwaasa wananchi kutoa ushirikiano kwa Jeshi la Polisi katika juhudi za kukomesha matukio hayo.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
PIX%2B2
Mkuu wa Wilaya ya Njombe, Ruth Msafiri akizungumza na wananchi  kuhusu matukio ya utekwaji na kuuliwa kwa watoto katika Mkoa wa Njombe, ambapo aliahidi kushirikiana na Vyombo vya Ulinzi na Usalama kukomesha matukio ya utekaji na kuuliwa kwa watoto.
PIX%2B3
Mkazi wa Njombe, Alex Msupilo akimuuliza maswali Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni(hayupo pichani), juu ya hatua zilizochukuliwa na Serikali kukagua leseni za waganga wa tiba asilia ambao wamekua wakitajwa kufanya tiba chonganishi zinazopelekea kutokea kwa matukio ya utekaji na kuuliwa kwa watoto katika mkoa huo.
PIX%2B4
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akizungumza katika kikao kidogo kilichohusisha Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Njombe na baadhi ya wananchi lengo ikiwa ni kujadili juu ya matukio ya utekaji na kuuliwa kwa watoto mkoani hapo.

No comments:

Post a Comment