Friday, November 2, 2018

SERIKALI YATILIA MKAZO KUBORESHA MAZINGIRA YA BIASHARA


1
Mkurungenzi wa uwezeshaji  sekta binafsi Ofisi ya Waziri Mkuu Bedason Sheranda akizungumza wakati wa kufungua mkutano wa mashauriano kati ya sekta binafsi na Serikali kuhusu mpango kazi jumuishi wa kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji nchini (CAP)  uliofanyika  jijini Dodoma alipokuwa mgeni rasmi kwa niaba ya Katibu Mkuu Ofisi Waziri mkuu Prof. Faustin Kamuzora
2
Oswaldo Mashindano toka Taasisi ya ya uatafiti wa kiuchumi na kijamii(ESRF) akisisitiza jambo kwa washiriki wa mkutano wa mashauriano kati ya sekta binafsi na Serikali kuhusu mpango kazi jumuishi wa kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji nchini (CAP)  uliofanyika  jijini Dodoma leo
3
Mjumbe wa Bodi ya Confederation Of Tanzania Industries (CTI) Dr Samuel Nyantahe akishiriki mkutano wa Serikali na Sekta Binafsi kuhusu mpango kazi jumuishi wa kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji nchini (CAP)  ulioitishwa na Ofisi ya Waziri Mkuu kwa kushirikiana na Taasisi ya ya uatafiti wa kiuchumi na kijamii(ESRF) uliofanyika Jijini Dodoma leo
E79A0770
Baadhi ya washiriki kutoka Sekta mbalimbali wakifuatilia maada katika  mkutano wa Serikali na Sekta Binafsi kuhusu mpango kazi jumuishi wa kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji nchini (CAP)ulioitishwa na Ofisi ya Waziri Mkuu kwa kushirikiana na Taasisi ya ya utafiti wa kiuchumi na kijamii(ESRF) uliofanyika Jijini Dodoma leo
E79A0797
Washiriki wakiwa na mgeni rasmi katika picha ya pamoja katika  mkutano wa Serikali na Sekta Binafsi kuhusu mpango kazi jumuishi wa kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji nchini (CAP) ulioitishwa na Ofisi ya Waziri Mkuu kwa kushirikiana na Taasisi ya ya utafiti wa kiuchumi na kijamii(ESRF) uliofanyika Jijini Dodoma leo
……………………..
Na.Alex Sonna wa Fullshangweblog,Dodoma
Serikali imedhamiria kuboresha mazingira ya kibiashara kwa sekta binafisi kwa kuchukua
hatua ambazo zimeanza kuonyesha mafanikio katika utoaji huduma za umma.
Hayo yamezungumzwa leo jijini Dodoma  na Katibu Mkuu Ofisi Waziri mkuu Prof. Faustin Kamuzora katika hotuba yake iliyosomwa na Mkurungenzi wa uwezeshaji sekta binafsi Bedason Sheranda, wakati wa kufungua mkutano wa mashauriano baina ya sekta binafsi na umma.
Prof.  Kamuzora  amesema kuwa kwa sasa Serikali imedhamiria kuboresha mazingira ya kibiashara kwa sekta binafsi kwa kuendelea kuchukua hatua ambazo zimesaidia kuonyesha mafanikio katika utoajia huduma kwa umma.
Mkutano huo umeandaliwa na Ofisi ya Waziri Mkuu kwa kushirikiana na Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF) kwa lengo la  kuboresha  mazingira ya biashara na wawekezaji
Katibu Mkuu amesema kuwa Serikali imeweka msukumo mkubwa katika kuongeza ufanisi kwenye utoaji wa huduma za umma kwa kuondoa rasimu usiokuwa wa lazima kwa kuweka mifumo ya kielektroniki ya malipo na utoaji wa huduma mbalimbali na kufuta kodi na tozo zilizokuwa kero kwa wafanyabiashara kwenye sekta mbalimbali kupitia bajeti ya Serikali ya mwaka 2017/18.
Kwa mujibu wa Katibu Mkuu amesema kuwa Serikali  imeandaa mwongozo wa utoaji wa leseni na vibali vya biashara kwa lengo la kurahisisha taratibu za leseni na vibali ,kupunguza kodi na tozo zisizo na tija ,na kuondoa mwingiliano wa kitaasisi katika udhibiti wa biashara.
Prof.Kamuzora amesema kuwa  maboresho mengine yaliyotekelezwa na Serikali ni pamoja na mfumo wa usajili wa biashara na kampuni kwa kuanzisha mfumo wa usajili kwa njia ya mtandao utakaoanza kutumika hivi karibuni .
Aliyataja maboresho hayo kuwa ni mpango wa kuboresha mazingira ya biashara Tanzania (BEST), mpango kazi wa kuboresha mazingira ya biashara kwa uwekezaji (ROADMAP) na mpango wa maboresho ya mfumo wa udhibiti wa biashara.
“Ubora wa mazingira ya biashara unategemea kasi ya Wizara na Taasisi za Serikali katika kuwekeza kwenye mifumo ya kielektroniki na kumarisha mawasiliano baina ya masjala na taasisi hizo ili kupunguza taratibu za kiutawala na hivyo kuwezesha upatikanaji kwa njia nyepesi ,gharama nafuu na kwa muda mfupi zaidi.”amesema Prof.Kamuzora
Prof.Kamuzora amesema kuwa,mafanikio katika kuboresha mazingira ya biashara yanahitaji mabadiliko makubwa ya kimtazamo na kifikra miongoni mwa watumishi wa serikali katika utoaji huduma wa sekta binafsi ili kuendana na kasi ya biashara.
Aidha amesema kuwa kwa  kupitia mkutano huo  wa mshaurinano kati ya sekta ya umma na sekta binafsi (PPD) unajumuisha pia wadau wengine  ambao ni Waratibu wa mazingira ya biashara, sekta mbalimbali za serikali na taasisi za utafiti na  elimu ya juu.
Amewataka wajumbe wa mkutano huo kila mmoja kwa nafasi yake kuona umuhimu wa Serikali kuiwezesha sekta binafsi kuwekeza na kufanya biashara kwa ajili ya manufaa mapana ya uchumi nchini ili kukuza miradi ya  biashara kwa sekta binafsi.
Kwa upande wake mjumbe wa bodi ya Baraza la Viwanda (CTI) Dk. Samuel Nyantahe amesema kuwa mpango kazi huo umechukua muda mrefu hivyo unahitaji utekekelezaji wake.
“Mambo yaliyoaanishwa kwenye mpango kazi huo ni mazuri lakini tunachotaka sekta binafsi ni utekelezaji wake ufanyike haraka kwani kuendendelea kuchelewa unasababisha nchi kushindwa kupaa kiuchumi”amesema Dk.Nyantahe
Dk,Nyantahe amesema kuwa mkakati wa kuboresha mazingira ya kibiashara Tanzania (BLUE PRINT)uliaanisha  changamoto nyingi  na kutoa majibu kwa matokeo ya majadiliano yaliyofanyika kati ya Sekta binafsi na Serikali.
Hata hivyo ameishukuru  Serikali kwa kuendelea kuandaa mikutano kati yao ambayo inasaidia kuboresha baadhi ya kero wanazoona kuwa na mvutano.

No comments :

Post a Comment