Mkurungenzi wa uwezeshaji sekta
binafsi Ofisi ya Waziri Mkuu Bedason Sheranda akizungumza wakati wa
kufungua mkutano wa mashauriano kati ya sekta binafsi na Serikali kuhusu
mpango kazi jumuishi wa kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji
nchini (CAP) uliofanyika jijini Dodoma alipokuwa mgeni rasmi kwa niaba
ya Katibu Mkuu Ofisi Waziri mkuu Prof. Faustin Kamuzora
Oswaldo Mashindano toka Taasisi ya
ya uatafiti wa kiuchumi na kijamii(ESRF) akisisitiza jambo kwa
washiriki wa mkutano wa mashauriano kati ya sekta binafsi na Serikali
kuhusu mpango kazi jumuishi wa kuboresha mazingira ya biashara na
uwekezaji nchini (CAP) uliofanyika jijini Dodoma leo
Mjumbe wa Bodi ya Confederation Of
Tanzania Industries (CTI) Dr Samuel Nyantahe akishiriki mkutano wa
Serikali na Sekta Binafsi kuhusu mpango kazi jumuishi wa kuboresha
mazingira ya biashara na uwekezaji nchini (CAP) ulioitishwa na Ofisi ya
Waziri Mkuu kwa kushirikiana na Taasisi ya ya uatafiti wa kiuchumi na
kijamii(ESRF) uliofanyika Jijini Dodoma leo
Baadhi ya washiriki kutoka Sekta
mbalimbali wakifuatilia maada katika mkutano wa Serikali na Sekta
Binafsi kuhusu mpango kazi jumuishi wa kuboresha mazingira ya biashara
na uwekezaji nchini (CAP)ulioitishwa na Ofisi ya Waziri Mkuu kwa
kushirikiana na Taasisi ya ya utafiti wa kiuchumi na kijamii(ESRF)
uliofanyika Jijini Dodoma leo
Washiriki wakiwa na mgeni rasmi
katika picha ya pamoja katika mkutano wa Serikali na Sekta
Binafsi kuhusu mpango kazi jumuishi wa kuboresha mazingira ya biashara
na uwekezaji nchini (CAP) ulioitishwa na Ofisi ya Waziri Mkuu kwa
kushirikiana na Taasisi ya ya utafiti wa kiuchumi na kijamii(ESRF)
uliofanyika Jijini Dodoma leo
……………………..
Na.Alex Sonna wa Fullshangweblog,Dodoma
Serikali imedhamiria kuboresha
mazingira ya kibiashara kwa sekta binafisi kwa kuchukua
hatua ambazo
zimeanza kuonyesha mafanikio katika utoaji huduma za umma.
Hayo yamezungumzwa leo jijini
Dodoma na Katibu Mkuu Ofisi Waziri mkuu Prof. Faustin Kamuzora katika
hotuba yake iliyosomwa na Mkurungenzi wa uwezeshaji sekta binafsi
Bedason Sheranda, wakati wa kufungua mkutano wa mashauriano baina ya
sekta binafsi na umma.
Prof. Kamuzora amesema kuwa kwa
sasa Serikali imedhamiria kuboresha mazingira ya kibiashara kwa sekta
binafsi kwa kuendelea kuchukua hatua ambazo zimesaidia kuonyesha
mafanikio katika utoajia huduma kwa umma.
Mkutano huo umeandaliwa na Ofisi
ya Waziri Mkuu kwa kushirikiana na Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na
Kijamii (ESRF) kwa lengo la kuboresha mazingira ya biashara na
wawekezaji
Katibu Mkuu amesema kuwa Serikali
imeweka msukumo mkubwa katika kuongeza ufanisi kwenye utoaji wa huduma
za umma kwa kuondoa rasimu usiokuwa wa lazima kwa kuweka mifumo ya
kielektroniki ya malipo na utoaji wa huduma mbalimbali na kufuta kodi na
tozo zilizokuwa kero kwa wafanyabiashara kwenye sekta mbalimbali
kupitia bajeti ya Serikali ya mwaka 2017/18.
Kwa mujibu wa Katibu Mkuu amesema
kuwa Serikali imeandaa mwongozo wa utoaji wa leseni na vibali vya
biashara kwa lengo la kurahisisha taratibu za leseni na vibali
,kupunguza kodi na tozo zisizo na tija ,na kuondoa mwingiliano wa
kitaasisi katika udhibiti wa biashara.
Prof.Kamuzora amesema kuwa
maboresho mengine yaliyotekelezwa na Serikali ni pamoja na mfumo wa
usajili wa biashara na kampuni kwa kuanzisha mfumo wa usajili kwa njia
ya mtandao utakaoanza kutumika hivi karibuni .
Aliyataja maboresho hayo kuwa ni
mpango wa kuboresha mazingira ya biashara Tanzania (BEST), mpango kazi
wa kuboresha mazingira ya biashara kwa uwekezaji (ROADMAP) na mpango wa
maboresho ya mfumo wa udhibiti wa biashara.
“Ubora wa mazingira ya biashara
unategemea kasi ya Wizara na Taasisi za Serikali katika kuwekeza kwenye
mifumo ya kielektroniki na kumarisha mawasiliano baina ya masjala na
taasisi hizo ili kupunguza taratibu za kiutawala na hivyo kuwezesha
upatikanaji kwa njia nyepesi ,gharama nafuu na kwa muda mfupi
zaidi.”amesema Prof.Kamuzora
Prof.Kamuzora amesema
kuwa,mafanikio katika kuboresha mazingira ya biashara yanahitaji
mabadiliko makubwa ya kimtazamo na kifikra miongoni mwa watumishi wa
serikali katika utoaji huduma wa sekta binafsi ili kuendana na kasi ya
biashara.
Aidha amesema kuwa kwa kupitia
mkutano huo wa mshaurinano kati ya sekta ya umma na sekta binafsi (PPD)
unajumuisha pia wadau wengine ambao ni Waratibu wa mazingira ya
biashara, sekta mbalimbali za serikali na taasisi za utafiti na elimu
ya juu.
Amewataka wajumbe wa mkutano huo
kila mmoja kwa nafasi yake kuona umuhimu wa Serikali kuiwezesha sekta
binafsi kuwekeza na kufanya biashara kwa ajili ya manufaa mapana ya
uchumi nchini ili kukuza miradi ya biashara kwa sekta binafsi.
Kwa upande wake mjumbe wa bodi ya
Baraza la Viwanda (CTI) Dk. Samuel Nyantahe amesema kuwa mpango kazi huo
umechukua muda mrefu hivyo unahitaji utekekelezaji wake.
“Mambo yaliyoaanishwa kwenye
mpango kazi huo ni mazuri lakini tunachotaka sekta binafsi ni
utekelezaji wake ufanyike haraka kwani kuendendelea kuchelewa
unasababisha nchi kushindwa kupaa kiuchumi”amesema Dk.Nyantahe
Dk,Nyantahe amesema kuwa mkakati
wa kuboresha mazingira ya kibiashara Tanzania (BLUE PRINT)uliaanisha
changamoto nyingi na kutoa majibu kwa matokeo ya majadiliano
yaliyofanyika kati ya Sekta binafsi na Serikali.
Hata hivyo ameishukuru Serikali
kwa kuendelea kuandaa mikutano kati yao ambayo inasaidia kuboresha
baadhi ya kero wanazoona kuwa na mvutano.
No comments:
Post a Comment