Msajili wa Hazina Bw. Athumani
Mbuttuka akizungumza wakati wa ufunguzi wa semina kwa Watendaji
Wakuu, Wenyeviti na wajumbe wa Bodi kuhusu usimamizi wa Taasisi na
mashirika ya Umma ili kuyawezesha kutimiza malengo ya kuanzishwa kwake.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya
Maendeleo ya Biashara Tanzania Bw. Edwin Rutageruka akizungumza wakati
wa semina kwa Watendaji Wakuu, Wenyeviti na wajumbe wa Bodi kuhusu
usimamizi wa Taasisi na mashirika ya Umma ili kuyawezesha kutimiza
malengo ya kuanzishwa kwake, Semina hiyo imeandaliwa na Ofisi ya Msajili
wa Hazina.
Msajili wa Hazina Bw. Athumani
Mbuttuka (katikati)akiwa kwenye picha ya pamoja na sehemu ya watendaji
wakuu wa mashirika ya umma walioshiriki katika semina kwa Watendaji
hao, Wenyeviti na wajumbe wa Bodi kuhusu usimamizi wa Taasisi na
mashirika ya Umma ili kuyawezesha kutimiza malengo ya kuanzishwa kwake.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya
Tiba ya Mifupa na Mishipa ya Fahamu (MOI) Dkt. Respicius Boniface
(kulia) akifuatilia hotuba ya Msajili wa Hazina Bw. Athumani Mbuttuka
wakati wa ufunguzi wa semina kwa Watendaji Wakuu, Wenyeviti na wajumbe
wa Bodi kuhusu usimamizi wa Taasisi na mashirika ya Umma ili kuyawezesha
kutimiza malengo ya kuanzishwa kwake.kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya
Wadhamini ya MOI Prof. Charles Anael Mkonyi.
Mwenyekiti wa Bodi ya Prof.
Humphrey Moshi akizungumza wakati wa wa semina kwa Watendaji Wakuu,
Wenyeviti na wajumbe wa Bodi kuhusu usimamizi wa Taasisi na mashirika ya
Umma ili kuyawezesha kutimiza malengo ya kuanzishwa kwake, Semina hiyo
imeandaliwa na Ofisi ya Msajili wa Hazina.
Sehemu ya Watendaji wakuu na
Wenyeviti na wajumbe wa Bodi wakifuatilia semina ya usimamizi wa
Taasisi na mashirika ya Umma ili kuyawezesha kutimiza malengo ya
kuanzishwa kwake, Semina hiyo imeandaliwa na Ofisi ya Msajili wa Hazina.
Picha zote na Frank Mvungi- MAELEZO
…………………….
Na: Frank Mvungi- MAELEZO
Msajili wa Hazina Bw. Athumani
Selemani Mbuttuka amewata Watendaji wakuu , Wenyeviti na Wajumbe wa Bodi
za Taasisi na mashirika ya umma kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia
Sheria, Kanuni, Taratibu na miongozo inayotolewa na Serikali .
Akizungumza katika Semina ya
kuwajengea uwezo Viongozi hao, Bw. Athumani amesem
a kuwa lengo la
Serikali ni kuona dhamira ya kuazishwa kwa Taasisi na Mashirika ya Umma
inafikiwa kwa wakati.
“Kwa mujibu wa vifungu Na.10 (2)
(e) na 10 (5) vya Sheria ya Msajili wa Hazina ina mamlaka ya Kusimamia
Bodi za Taasisi na Mashirika ya Umma hivyo, tuna wajibu wa kuhakikisha
kuwa Bodi na Viongozi wote wanaelewa majukumu yao kwa mujibu wa sheria,
kanuni na taratibu”; Alisisitiza Mbutuka.
Akifafanua amesema kuwa Bodi na
Watendaji wakuu wanapaswa kuwa makini, wabunifu na kufanya maamuzi
sahihi na kwa wakati ili kuhakikisha kuwa Taasisi zinajiwekea mikakati
ya kupunguza gharama za uendeshaji zinazotokana na matumizi yasiyo ya
lazima hususani safari za Bodi na viongozi zisizokuwa na manufaa kwa
Taasisi husika.
Alibainisha kuwa Taasisi zinapaswa
kuwa na mikakati madhubuti ya kukusanya mapato ili kutekeleza majukumu
yake kwa ufanisi, sambamba na kuhakikisha kuwa matumizi yote yanafanyika
kwa kuzingatia Sheria, Kanuni na miongozo mbalimbali ya Serikali.
“Taasisi zenye utendaji
usioridhisha na zile zinazopata hasara kila mwaka, kuweni wabunifu na
kuweka mikakati ya kuboresha utendaji na pia kuhakikisha kuwa, hoja za
ukaguzi ( CAG,IAG, TR na PPRA) na maagizo ya kamati za Bunge yawekewa
mkakati thabiti na zinatekelezwa ipasavyo na kwa wakati;” Amebainisha
Mbutta.
Akizungumzia Taasisi zinazopaswa
kuchangia asilimia 15 ya mapato ghafi katika mfuko mkuu wa Serikali
zinatekeleza wajibu huo kwa mujibu wa sheria kila robo mwaka,Bodi
inatakiwa kuhakkisha kuwa, mchango unaowasilishwa ni sahihi na unaendana
na kiwango cha mapato ghafi ya Taasisi husika au shirika.
Alisema kuwa upande wa matumizi
hasa katika malipo ya posho, marupurupu, na maslahi mbalimbali ya Bodi,
Viongozi wa Taasisi na Watumishi yanapaswa kuzingatia sheria, kanuni na
miongozo ya Serikali.
Aliongeza kuwa malipo ya posho za
nyumba, posho za simu na umeme yanapaswa kulipwa kwa watumishi wenye
stahili hizo kisheria tofauti na ilivyo sasa ambapo baadhi ya Taasisi
zinaendakinyume na utaraibu huo.
Pia aliwata Watendaji wakuu na Bodi kutofanya malipo kwa kutumia nyaraka ambazo hazijaidhinishwa na Ofisi ya Msajili wa Hazina.
Ofisi ya Msajili wa Hazina
inafanya kazi kwa ushirikiano ili kujenga Taasisi zinazoendana na
Dhamira ya Serikali ya Awamu ya Tano ambazo ni madhubuti, Bora na
endelevu kwa maslahi ya wananchi wote na Taifa kwa ujumla.
Ofisi ya Msajili wa Hazina
imeratibu mafunzo hayo kwa Watendaji Wakuu, Wenyeviti na Wajumbe wa Bodi
za Taasisi na Mashirika ya Umma 17 kwa lengo la kuwajengea uwezo katika
utendaji wao wa kusimamia taasisi hizo ili kuongeza ufanisi.
No comments:
Post a Comment