WAZIRI
MKUU Kassim Majaliwa amesema Tanzania inaongoza kwa kupokea uwekezaji
wa kigeni wa moja kwa moja katika Ukanda wa Afrika ya Mashariki.
“Mtiririko
wa uwekezaji wa kigeni wa moja kwa moja nchini umeongezeka kwa zaidi ya
miaka 10 iliyopita na sasa wawekezaji wameipa kipaumbele Tanzania kama
kitovu cha uwekezaji barani Afrika.”
Ameyasema
hayo leo (Jumapili, Septemba 02 ,2018) wakati akihutubiaKongamano la
Biashara kati ya Tabnzania na China kwenye Hoteli ya Winstin jijini
Beijing nchini China.
Waziri
Mkuu amesema Tanzania imethibitika kuwa ni Taifa lililodhamiria kwa
dhati kujenga uchumi wa viwanda , pamoja na kulinda na kudumisha amani
na utulivu.
Amesema
ripoti ya uwekezaji duniani iliyotolewa mwaka 2018, inaonesha kuwa
Tanzania inaongoza kwa kupokea uwekezaji katika ukanda wa Afrika ya
Mashariki na imepokea kiasi cha Dola za Marekani bilioni 1.2 mwaka 2017.
Waziri
Mkuu amesema Tanzania inafanya juhudi kubwa ili iweze kuwa nchi ya
uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025, hivyo imeweka mkazo mkubwa
katika kujenga msingi imara wa viwanda.
“Ili
kufanikisha hilo tumeandaa Ukanda wa Kuzalisha kwa ajili ya mauzo ya
Nje na Ukanda maalum wa Kiuchumi tukilenga kutimiza mkakakati wetu wa
kukuza uchumi wa viwanda na biashara.”
Akizungumzia
kuhusu sekta ya fedha, Waziri Mkuu amesema Tanzania inawakaribisha
wawekezaji kuanzisha Taasisi za Kifedha kama vile benki kwa ajili ya
kutoa mikopo midogo midogo, benki za uwekezaji, benki za kilimo na benki
za biashara.
Kuhusu
uwekezaji kutoka China uliosajiliwa na Kituio cha Uwekezaji Tanzania
(TIC) kati ya Novemba 2015 hadi Oktoba 2017, Waziri Mkuu
amesema umefikia thamani ya Dola za Marekani bilioni 1.077 na umejikita
katika meneo ya kilimo, majengo ya biashara, rasilimali watu, viwanda
na utalii.
Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu amesemakuna
fursa nyingi kwenye sekta ya huduma hususan katika Teknolojia ya Habari
na Mawasiliano (TEHAMA) ambayo ni miongoni mwa sekta ndogo zinazokuwa
kwa haraka nchini Tanzania.
Pia
kumekuwa na ukuaji na mageuzi ya haraka katika soko la TEHAMA nchini
kwa miaka 10 iliyopita. “Soko la Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
limekuwa kwa ongezeko la watumiaji, aina ya huduma zinazotolewa pamoja
na kupanuka kwa eneo ambalo huduma hizo hutolewa.”
Waziri
Mkuu ameongeza kuwa, “Tanzania kuna fursa zisizo na ukomo katika eneo
hili huku kukiwa na matarajio ya kukuwa kwa soko la kikanda.”
“Maeneo
ya kuwekeza ni pamoja na utoaji wa huduma za simu hususan katika maeneo
ya vijijini, utoaji na uendeshaji wa huduma za mtandao pamoja na
ukarabati na matengenezo ya vifaa vya mawasiliano. Tunawakaribisha
wawekezaji kuwekeza katika maeneo haya.”
Amesema
kwa wale ambao nia yao ni kuwekeza katika kilimo, Tanzania ina hekta
milioni 44 za ardhi inayofaa kwa kilimo na takribani hekta milioni 29.4
kwa ajili ya umwagiliaji.
“Ninawakalibisha wawekezaji kuja kuwekeza katika kilimo cha biashara
kwa mazao kama miwa, mpunga, ngano, kahawa, chai na mahindi. Tuna fursa
kubwa ya kuwekeza katika kilimo cha miwa na uzalishaji wa sukari.”
Waziri
Mkuu Kassim Majaliwa akisalimiana na baadhi ya Wajumbe kutoka Tanzania
waliopo nchini China kuhudhudhuria Mkutano wa wakuu wa nchi na serikali
wa Jukwaa la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC),unaotarajiwa
kufunguliwa na Rais wa China Xi Jinping kesho jumatatu Septemba 3, 2018.
|
No comments :
Post a Comment