Sunday, September 2, 2018

SERIKALI YATOA RAI KWA WAAJIRI KUBUNI PROGRAM ZA UKUZAJI UJUZI KWA WAFANYAKAZI WAO.





Serikali imetoa rai kwa waajiri nchini kuanzisha programu mbalimbali za ukuzaji ujuzi ili kuendeleza nguvukazi yenye ujuzi stahiki na shindani katika soko la Ajira,Rai hiyo imetolewa  na Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi,Vijana na Ajira Mh Anthony Mavunde  alivyokuwa akifungua Kituo cha Ukuzaji ujuzi cha Kiwanda cha Kagera Sugar katika Wilaya ya Missenyi,Mkoani Kagera.

Naibu Waziri Mavunde amekipongeza kiwanda cha Kagera Sugar kwa kuanzisha kituo cha kuendeleza ujuzi wa wafanyakazi wake na kuwashukuru kwa utekelezaji wa programu ya kuajiri wanavyuo moja kwa moja kutoka vyuoni pasipo kujali sharti la UZOEFU ambapo jumla ya wanachuo 250 wamenufaika na mpango huu.

Aidha Naibu Waziri Mavunde amefurahishwa pia na namna Vijana wa Wilaya ya Missenyi walivyochangamkia fursa ya kilimo cha miwa kama wakulima wadogo wadogo “*Outgrowers*” na kuahidi kuwaunganisha na mifuko ya Uwezeshwaji ili Vijana wengi zaidi wapate mikopo ya kuendeleza kilimo hicho.

Akimkaribisha Mgeni Rasmi,Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Kagera Sugar Ndg Seif A.Seif ameahidi kuendelea kuwekeza katika wafanyakazi wake kwa kuwajengea ujuzi stahiki na kuahidi kuendelea kuwaajiri moja kwa moja Vijana wanaotoka vyuoni bila kuweka sharti la uzoefu na badala yake watawasaidia vijana hao kupata ujuzi na uzoefu wakiwa tayari katika Ajira

No comments :

Post a Comment