Serikali
imetoa rai kwa waajiri nchini kuanzisha programu mbalimbali za ukuzaji ujuzi
ili kuendeleza nguvukazi yenye ujuzi stahiki na shindani katika soko la
Ajira,Rai hiyo imetolewa na Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri
Mkuu-Kazi,Vijana na Ajira Mh Anthony Mavunde
alivyokuwa akifungua Kituo cha Ukuzaji ujuzi cha Kiwanda cha Kagera
Sugar katika Wilaya ya Missenyi,Mkoani Kagera.
Naibu
Waziri Mavunde amekipongeza kiwanda cha Kagera Sugar kwa kuanzisha kituo cha
kuendeleza ujuzi wa wafanyakazi wake na kuwashukuru kwa utekelezaji wa programu
ya kuajiri wanavyuo moja kwa moja kutoka vyuoni pasipo kujali sharti la UZOEFU
ambapo jumla ya wanachuo 250 wamenufaika na mpango huu.
Aidha
Naibu Waziri Mavunde amefurahishwa pia na namna Vijana wa Wilaya ya Missenyi
walivyochangamkia fursa ya kilimo cha miwa kama wakulima wadogo wadogo
“*Outgrowers*” na kuahidi kuwaunganisha na mifuko ya Uwezeshwaji ili Vijana
wengi zaidi wapate mikopo ya kuendeleza kilimo hicho.
Akimkaribisha Mgeni Rasmi,Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Kagera Sugar Ndg Seif A.Seif ameahidi kuendelea kuwekeza katika wafanyakazi wake kwa kuwajengea ujuzi stahiki na kuahidi kuendelea kuwaajiri moja kwa moja Vijana wanaotoka vyuoni bila kuweka sharti la uzoefu na badala yake watawasaidia vijana hao kupata ujuzi na uzoefu wakiwa tayari katika Ajira
No comments:
Post a Comment