Treni
ya ROVOS iliyobeba watalii 64 wa Kijerumani kutoka Afrika ya Kusini, ikiwasili
leo stesheni ya TAZARA Jijini Dar es Salaam.
Mama
wa Kijerumani Linde Erdmann (katikati) akifurahia kuwasili Tanzania kwa mara ya
kwanza akitokea Afrika ya Kusini kwa kutumia treni ya ROVOS kupitia reli ya
TAZARA.
Meneja
Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania na Zambia (TAZARA) Fuad Abdallah (kulia), akizungumza
na Waandishi wa Habari katika makao makuu ya shirika hilo Jijini Dar es Salaam
kabla ya kuwasili kwa treni ya kitalii ya ROVOS kutoka Afrika ya Kusini.
Baadhi
ya watalii kutoka Ujerumani wakifurahia buradani ya bendi ya Polisi baada ya
kushuka kutoka kwenye treni ya ROVOS moja kati ya treni ya kifahari duniani, watalii
hao wamekuja nchini kutembelea vivutio mbalimbali.
Meneja Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania na Zambia (TAZARA) Fuad
Abdallah (mwenye fulana nyekundu) akifuatilia mahojiano baina ya watalii na
Afisa Habari wa Idara ya Habari-MAELEZO, Abraham Nyantori .
Mtalii
Diesknahn akizungumza na Afisa Habari wa Idara ya Habari Fatma Salum (kushoto) mara
baada ya kuwasili nchini na treni ya ROVOS wakitokea Afika ya Kusini.
Moja
ya mgahawa unaopatikana katika treni ya kifahari ya ROVOS iliyowasili leo hapa
nchini ikitokea Afrika ya Kusini kupitia reli ya TAZARA.
Dereva
wa treni ya ROVOS Abby (kulia) akizungumza na mmoja wa wafanyakazi wa treni
hiyo mara baada ya kuwasili katika stesheni ya Dar es Salaam ikitokea
Afrika ya kusini kupitia reli ya TAZARA.
Moja
ya chumba cha kupumzika abiria katika treni ya kifahari ya ROVOS, treni hiyo ni
miongoni mwa treni tatu za kifahari duniani.
No comments:
Post a Comment