Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu
Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na watu wenye Walemavu, Mhe. Jenista Mhagama
(Mb), akuzungumza wakati akiahirisha semina ya Ubia kati ya Sekta ya Umma na
Sekta Binafsi (PPP) yaliyoandaliwa na Wizara ya Fedha na Mipango kwa
kushirikiana na Benki ya Dunia, Jijini Dodoma.
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango,
Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb), akifungua semina ya siku moja iliyowahusisha
Mawaziri, Naibu Mawaziri na viongozi wengine waandamizi wa Serikali na Taasisi
zake, kuhusu Ubia Sekta ya Umma na Binafsi (PPP), iliyofanyika katika ukumbi
wa Kambarage, Wizara ya Fedha na
Mipango, Jijini Dodoma.
Mshauri wa Masuala ya Kisheria katika
mradi wa Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPP) kutoka Benki ya
Dunia, Philip Kelly akiwasilisha mada katika semina ya siku moja ya PPP, iliyofanyika katika ukumbi wa Wizara ya
Fedha na Mipango, Jijini Dodoma.
Mshauri wa Masuala ya Kisheria katika
mradi wa Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPP) Bw. Philip Kelly
(katikati) akifafanua jambo wakati wa semina ya siku moja ya PPP, iliyofanyika katika ukumbi wa Wizara ya
Fedha na Mipango, Jijini Dodoma. Kushoto ni Mtaalamu wa Masuala ya PPP, Bw. Craig
Sugden na kulia ni Bw. Abhijit Bhaumik, wote watatu wanatoka Benki ya Dunia.
Waziri wa mambo ya Ndani ya Nchi,
Mhe. Kangi Lugola (Mb) (kulia) akiwa na Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha
Mapinduzi -CCM (2015) wakati aliposhiriki semina ya Siku moja iliyohusisha
Mawaziri, Naibu Mawaziri na viongozi wengine waandamizi wa Serikali na Taasisi
zake, kuhusu Ubia Sekta ya Umma na Binafsi (PPP), iliyofanyika katika ukumbi wa Kambarage,
Wizara ya Fedha na Mipango, Jijini Dodoma. Kushoto ni Naibu Waziri wa fedha na
Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb).
Baadhi ya Washiriki wa Semina ya siku
moja iliyohusisha Mawaziri, Naibu Mawaziri na viongozi wengine waandamizi wa
Serikali na Taasisi zake, wakifuatilia mada kuhusu Ubia Sekta ya Umma na
Binafsi (PPP), iliyofanyika katika ukumbi wa
Kambarage, Wizara ya Fedha na Mipango, Jijini Dodoma.
Kamishna wa Idara ya Ubia Sekta ya
Umma na Binafsi (PPP), Wizara ya Fedha na Mipango, Dkt. John Mboya, akieleza
namna Serikali na Sekta Binafsi ilivyojipanga kutekeleza zaidi ya miradi 10
katika sekta za Afya, Barabara, Reli, Dawa za binadamu na elimu, wakati wa
Semina ya siku moja ya Ubia kati ya pande hizo mbili iliyowashirikisha
Mawaziri, Naibu Mawaziri na Maafisa waandamizi wa Serikali na baadhi ya Taasisi
zake, Jijini Dodoma
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu
Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na watu wenye Walemavu, Mhe. Jenista Mhagama
(Mb), (kushoto) akisoma makabrasha kuhusu Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta
Binafsi (PPP) yaliyoandaliwa na Wizara ya Fedha na Mipango kwa kushirikiana na
Benki ya Dunia, Jijini Dodoma. kushoto kwake ni Naibu Waziri Wizara ya Viwanda,
Biashara na Uwekezaji Mhe. Mhandisi Stella Manyaya (Mb) na anayefuatiwa ni
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Japhet Hasunga.
Washiriki wakiwa katika picha ya
pamoja baada ya kuahirishwa kwa Semina ya Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta
Binafsi (PPP) yaliyoandaliwa na Wizara ya Fedha na Mipango kwa kushirikiana na
Benki ya Dunia, yaliyohusisha Mawaziri
na Manaibu waziri, Jijini Dodoma.(Picha na Kitengo Cha
Mawasiliano Serikalini-WFM)
Na Benny Mwaipaja, WFM,
Dodoma
Serikali ya Tanzania
imepiga hatua kubwa katika kuanzisha na kutekeleza miradi mikubwa ya maendeleo
kwa ubia kati ya Sekta ya Umma na Binafsi
(PPP) ambapo miradi zaidi ya 11 iko
katika hatua mbalimbali za utekelezaji lengo likiwa ni kufanikisha azma ya kuwa na uchumi wa viwanda.
Hayo yamesemwa na Kamishna
wa Idara ya Ubia Sekta ya Umma na Binafsi
(PPP), Wizara ya Fedha na Mipango, Dkt. John
Mboya wakati akiwasilisha mada ya
utekelezaji wa dhana ya ushirikishwaji wa sekta binafsi katika miradi ya maendeleo
nchini kwenye semina iliyowashirikisha mawaziri, naibu mawaziri na baadhi ya
watendaji wa serikali iliyofanyika kwenye ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango
jijini Dodoma.
Akiwasilisha mada hiyo,
Dkt. John Mboya amesisitiza umuhimu wa kuwepo kwa umakini mkubwa katika uandaaji na utekelezaji
wa dhana hiyo ya ubia Sekta ya Umma na Binafsi kwa kuzingatia sheria, sera,
miongozo, kanuni na taratibu mbalimbali zilizopo.
Aidha alizitaka taasisi na
wadau wa utekelezaji kuwa tayari kujifunza kutoka katika nchi zilizoendelea kupitia
dhana hii ya ushirikikishwaji wa sekta binafsi katika kuchochea ukuaji wa
viwanda na uchumi wa nchi kwa ujumla.
Dkt.
Mboya aliitaja baadhi
ya miradi iliyoko katika hatua mbalimbali ya utekelezwaji kwa Ubia kati
ya Sekta ya Umma na Binafsi kuwa ni mradi wa mabasi yaendayo haraka
(DART), Ujenzi
wa Viwanda vya dawa, mradi wa VETA utakaohusisha ujenzi wa vyuo 10
ambavyo
vinatarajiwa kutoa ujuzi mbalimbali kwa wanafunzi wapatao 90,000 ili
kukidhi
mahitaji ya wataalamu watakao saidia kufanikisha uchumi wa viwanda.
"MIradi Mingine ni Ujenzi
wa Bandari ya Mwambani, barabara ya Dar es salaam hadi Chalinze, Ujenzi wa Reli
kwenye miradi ya Mchuchuma hadi Mbambabay mikoa ya Kusini ya Lindi na Mtwara,
Ujenzi wa Reli kuanzia Tanga, Arusha hadi Musoma, na mradi wa umeme wa Chuo Kikuu cha Dodoma.
Akijibu swali la Naibu
Waziri Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Josesph Kakunda, aliyetaka kujua kuhusu
kuondolewa kwa sheria ya utekelezwaji wa
miradi kwa Ushirikishwaji wa Pamoja kati ya serikali na sekta binafsi (Joint
Venture) ambayo haikufanikiwa kama ilivyokusudiwa hapo awali, Dkt. Mboya
alisema kuwa sheria hiyo haijaondolewa bali miradi hiyo itatekelezwa kupitia sheria ya
Kampuni.
Akichangia katika mjadala
wa semina hiyo, Naibu Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhandisi Stella
Manyanya, alisema ni vema wakati wa kuchagua miradi wahusika wawe makini ili
kuepuka kuanzisha miradi inayofanana na ambayo inaweza kuwa chanzo cha kufa kwa
miradi iliyotangulia.
"Ninashauri kuwepo
kwa fursa ya ushirikishwaji katika miradi midogo ambayo ina manufaa kwa
wananchi ikiwemo ya ujenzi wa nyumba za waalimu" Alisema Mhandisi Manyanya
Naibu Waziri wa Mifugo na
Uvuvi, Abdallah Ulega, alizitaka taasisi ambazo zinatekeleza miradi kwa ubia na
sekta binafsi zielezee umma wa watanzania mafanikio yaliyopatikana ili
kuhamasisha wadau wengine kufuata nyayo hizo huku akitolea mfano Shirika la Maendeleo ya Petroli
nchini (TPDC) ambalo nalo liko katika
utekelezaji wa dhana hiyo.
Mwenyekiti wa semina
hiyo Naibu Waziri wa Fedha na Mipango,
Dkt. Ashatu Kijaji, alisema kuwa Serikali imepeleka Muswada Bungeni unaohusu PPP,
ambao ukipitishwa na Bunge linalotarajiwa kuanza Septemba 4, 2018, utekelezaji
wa ubia huo utakwenda kwa kasi zaidi ili kuiwezesha nchi kufikia malengo yake
ya kukuza uchumi na kuleta maendeleo ya wananchi.
Kwa upande wake, Waziri wa
Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge , Kazi,Vijana, Ajira na Walemavu, Jenister
Mhagama, akiahirisha mafunzo hayo, aliwataka wadau wa semina hiyo kuendelea
kukutana na kuelimishana hadi hapo marekebisho ya sheria hiyo ya Ubia Sekta ya
Umma na Binafsi (PPP) yatakapofanyika.
"Utekelezwaji wa
dhana hii ya Ubia Sekta ya Umma na Binafsi ndio njia rahisi itakayosaidia
kukamilisha miradi mingi ambayo imeainishwa katika ilani ya uchaguzi ya Chama
Cha Mapainduzi (CCM) na kwenye Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano, bila
ushirikiano huu na sekta binafsi hatuwezi kufikia uchumi wa viwanda kwa kasi
inayotakiwa’’ Alisema Waziri Mhagama.
Semina hiyo ya siku moja
imeendeshwa na wataalamu wa masuala ya Ubia Sekta ya Umma na Binafsi kutoka
Benki ya Dunia, ambapo Jumapili, kamati tatu za Bunge zitapatiwa elimu na
kujengewa uwezo kuhusu dhana hiyo ya PPP.
No comments:
Post a Comment