NAIBU
Waziri Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano,
Mhandisi Atashasta Nditiye, (kushoto), akiwa na Mkurugenzi Mkuu wa
Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Bw.Richard Mayongela,
akizungumza na waandishi w ahabari kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa
wa Dar es Salaam, Agosti 30, 2018.
NA
K-VIS BLOG, Khalfan Said
NAIBU
Waziri Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano,
Mhandisi Atashasta Nditiye, ameagiza Mamlaka
ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), kwa kushirikiana na Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya
Ilala, kukagua viwanja 537 vilivyotengwa huko Msongola, kwa ajili ya waliokuwa
wakazi wa eneo la Kipawa jijini Dar es Salaam Jumanne wiki ijayo ili
kujiridhisha kama viwanja hivyo vipo na vinafaa.
Mhandisi
Nditiye ametoa agizo hilo leo Agostri 30, 2018, wakati akizungumza na waandishi
wa habari kwe nye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es
Salaam ambapo alieleza wasiwasi wake kuwa kampuni iliyopewa kandarasi ya
kuwatafutia viwanja wananchi hao haijatekeleza wajibu wake ipasavyo licha ya
kuwa tayari imelipwa kiasi cha shilingi bilioni 3.7.
“Nakuagiza
Mkurugenzi wa TAA, kwa kushirikiana na Mkurugenzi wa Wilaya Jumanne ijayo
muende mkakague eno hilo la viwanja 537 muone kama vipo kwa sababu kumekuwa na
shida sana na hawa wenzetu wa Tanzania
Remix Centre nyinyi wenyewe mnajua, kuna
shida ya miundombinu, sasa lazime mjue eneo hilo linafikika, na viwanja hivyo
vinajengeka.” Alisema
Alisema
Wananchi wako tayari kushirikiana na serikali katika kuhakikisha upanuzi wa
uwanja unakwenda vizuri.
Kampuni
ya Tanzania Remix Centre ilipendekezwa na Manispaa ya Ilala na kupewa kandarasi ya kutafuta viwanja kwa ajili ya makazi
mapya ya wananchi waliokuwa wakiishi eneo la Kipawa jijini Dar es Salaam.
Hata
hivyo kulikuwepo na mivutano kati ya Mamlaka na Wananchi ambapo baadhi yao
walipeleka shauri hilo mahakamani na hiovyo kufanya zoezi hilo la kuwahamisha
wananchi hao kwenye eneo hilo jipya kusuasua.
Hata
hivyo akitoa taarifa kwa Mhe. Naibu Waziri Nditiye, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka
ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Bw.Richard Mayongela alisema, Novemba
mwaka jana, TAA ilikutana na wadau wakiwemo wananchi, Manispaa ya Ilala, Ofisi
ya Mkuu wa Wilaya na Kampuni iliyoingia ubia na Manispaa ya Ilala katika
kutafuta viwanja kwa ajili ya wananchi hao.
“Mradi
huu ulihusisha upatikanaji wa viwanja 1,600 kwa mujibu wa mkataba wa awali
ambapo fidia yake ilipaswa kufanywa kwa awamu mbili ya watu 800, hata hivyo kwa
mujibu wa sheria kipinde kile ilitaka mwananchi apewe eneo lakini alipwe fidia
pia.” Alisema na kufafanua kuwa.
“Sasa
wananchi wa Kipawa na Kigilagila walilipwa fidia kwa mujibu wa sheria na kwao
hakukuwa na tatizo, kwa maana walipewa fedha taslimu na viwanja maeneo ya Pugu
Mwakanga.” Alisema Bw. Mayongela
Akieleza
zaidi Bw. Mayongela alsiema Baada ya kufanya tathmini, ilibainika kuwa wananchi
wa Kipunguni A na Kipunguni Mashariki ambapo kulikuwa na viwanja 1,186 baada ya
kufanya tathmini viwanja vilivyohitajika siyo 1,600, bali ni 1,186, kwa ajili
ya fidia ya wananchi wa maeneo hayo mawili na katika viwanja hivyo viwanja 537
serikali ilishatoa kiasi cha shilingi bilioni 3.7 ili kutekeleza zoezi hilo.
Sisi
kwa kushirikiana na mbia wa Mnaispaa ya Ilala yaani Tanzania Remix Centre, tukaandaa vile viwanja na viwanja vile
vimeshapatikana na kuanzia hivi sasa, viwanja hivyo vitagawiwa kwa wananchi.
Aidha
katika hatua nyingine, Mhe. Nditiye amesema wakati umefika sasa kwa Mamlaka ya
Viwanja vya Ndege, kuanzisha kitengo cha Estate ili kihakikisha viwanja vyake
vyote nchini vinakuwa na hati miliki.
“Unda
kitengo cha Estate kisichozidi watu 10 ili kihakikishe kila kiwanja kinachomilikiwa
na TAA kinakuwa na hati nah ii itaepusha migogoro na wananchi.” Alisema
Kandoni
na maagzio hayo, Naibu Waziri, ameondoka nchini leo kuelekea Burundi kwa ajili
yanuzinduzi wa safari ya kwanza ya ndege za ATCL zitakazoanza safari zake
Darves Salaam kwenda Bunjumbura.
Mhe.
Nditiye amefuatana na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Miundombinu, Mhe. Selemani
Moshi Kakoso na baadhi
ya wajumbe wa kamati hiyo
Mkurugenzi
Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Bw.Richard
Mayongela, (kulia), akitoa taarifa kwa Naibu Waziri Mhe. Nditiye
NAIBU
Waziri wa Mawasiliano na Uchukuzi,
Mhandisi Atashasta Nditiye, (kushoto), akipeana mikono na Mwenyekiti w
aKamati ya Bunge ya Miundombinu, Mhe. Suleiman Moshi Kakoso muda mfupi
kabla ya kuondoka kuelekea Bunjumbura Burundi kwenye uzinduzi wa safari
za ndege za ATCL nchini humo. Katikati, ni mjumbe wa Kamati Mhe. Daniel
Nsanzugwanko.
Mkurugenzi Mkuu wa TAA, Bw. Richard
Mayongela, akifafanua Zaidi wakati wa mkutano huo. Wapili kushoto ni
Mkurugenzi wa Kiwanja cha ndege cha Julius Nyerere, Bw. Paul Rwegasha.
na Mwakilishi kutoka Mnaispaa ya Ilala.
Mwakilishi kiutoka Manispaa ya Ilala,Bw.Nicodemus Shirima akifafanua masuala mbalimbali kuhusu viwanja hivyo.
Mkurugenzi wa kampuni ya Tanznaia Remix Centre, iliyopewa kandarasi ya kutafuta viwanja, Bi.Rosemary Shimata, akizunguzma.
Mkurugenzi Mkuu wa TAA, Bw. Richard Mayongela, akifurahia jambo na Inspekta wa polisi Daniel Mwakibete, baada ya mkutano huo.
Naibu Waziri Nditiye, (kushoto),
Mkurugenzi Mkuu wa TAA, Bw. Mayongela, (katikati), wakijadiliana jambo
na mwakilishi kutoka ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Bw.Nicodemus
Shirima
No comments :
Post a Comment