Bw.Richard Mayongela |
NA MWANDISHI WETU
BODI
ya Ushauri (MAB) ya Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), imempongeza
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo Bw. Richard Mayongela kwa kuthibitishwa rasmi
katika nafasi hiyo.
Awali
Bw. Mayongela alikuwa akikaimu nafasi hiyo kwa takribani miezi 11 iliyopita.
Pongezi
hizo zimetolewa na Mwenyekiti wa MAB, Mhandisi Prof. Ninatubu Lema kwa niaba ya
bodi nzima amesema "Nimepokea taarifa rasmi ya kuthibitishwa kwako kuwa
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania.
Ninakupongeza."
Mhandisi
Prof. Lema amesema kutokana na wadhifa huo, anatumaini makubwa Mkurugenzi huyo
ataendelea kuiongoza Mamlaka hiyo kwa utendaji makini na kwa weledi wa hali ya
juu unaozingatia ufanisi na uadilifu usio na shaka yoyote.
Pia
amemtaka Bw. Mayongela kujenga timu yenye nguvu kwenye Mamlaka
itakayoongozwa
kwa misingi ya dira sahihi na mwelekeo mmoja kwa wote, unaoheshimu na kuzitumia
fani za kila mtumishi wa Mamlaka ipasavyo kwa manufaa mapana ya Taifa.
"Mungu
akuzidishie hekima katika majukumu yako," amesema Mhandisi Prof. Lema.
Uthibitisho
huo uliwasilishwa na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Issac
Kamwelwe na kusomwa katika mkutano wa Mameneja wa Viwanja vya Ndege Tanzania
uliofanyika hivi karibuni Jijini Dar es Salaam na Kaimu Mkurugenzi wa
Rasilimali Watu na Utawala, Bw. Lawrence Thobias.
Halikadhalika,
Bw. Mayongela baada ya uthibitisho huo rasmi aliwashukuru
Watumishi
wote wa Mamlaka na kusema hatua hiyo imechangiwa na juhudi za pamoja na
ushirikiano kwa kipindi chote cha takribani miezi 11 alichokuwa akikaimu nafasi
hiyo.
"Bila
nyie nisingeweza kufanya kitu chochote, na hali kadhalika bila ushirikiano wenu
peke yangu nisingeweza," amesema Bw. Mayongela.
Hatahivyo
amewasisitizia Watumishi wenzake kuchapa kazi kwa weledi, bidii, maarifa na
uzalendo mkubwa usioweza kutiliwa mashaka ya aina yoyote kwa kuwahudumia Wadau
na Watanzania wote kwa ujumla ili kuleta tija kubwa kwa Taifa.
No comments :
Post a Comment