Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akiagana na mgeni wake Waziri Mkuu wa Jamhuri ya
Korea, Lee Nak-yon wakati alipoondoka kwenye uwanja wa ndege wa Julius
Nyerere jijini Dar es salaam baada ya ziara ya siku tatu nchini, Julai
23, 2018.
NA OWM, DAR ES SALAAM
WAZIRI MKUU wa Jamhuri ya
Korea, Lee Nak-yon amemaliza ziara yake ya kiserikali ya siku tatu hapa nchini
na kusindikizwa na mwenyeji wake, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.
Waziri Mkuu
huyo wa Korea ambaye ameondoka leo
(Jumatatu, Julai 23, 2018) saa 9.14 alasiri, ameelekea Oman ambako atakuwa na
ziara ya kikazi ya siku mbili. Aliwasili nchini juzi akitokea Kenya ambako pia
alikuwa na ziara ya siku mbili.
Katika uwanja
wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere, Waziri Mkuu wa Korea Kusini alisindikizwa
pia na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Dk. Augustine
Mahiga, Naibu
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Eng. Stella Manyanya na viongozi wa
mkoa wa Dar es Salaam
Kabla ya
kuondoka alishuhudia burudani kutoka vikundi vya ngoma na matarumbeta uwanjani
hapo.
Mara baada ya mgeni wake
kuondoka, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alizungumza na wasanii waliokuwepo
uwanjani na kuwapongeza kwa kujitokeza kutoa burudani kila wakati wageni wanapoitembelea
Tanzania.
“Tunawashukuru sana wasanii kwa
sababu mlikuja wakati wa mapokezi ya mgeni wetu na sasa mmekuja tena kumsindikiza.
Mgeni wetu amefurahia sana ngoma zetu na amesema atarudi tena Tanzania.”
“Kwa niaba ya Ofisi ya Waziri
Mkuu na Serikali kwa ujumla, tunatambua kuwa mnajitoa muda wenu kila mnapokuja
kupokea na kusindikiza wageni ili kuweka sura nzuri ya Taifa letu wakati wa
kupokea wageni wetu, tunawashukuru sana,” amesema.
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akiagana na mgeni wake Waziri Mkuu wa Jamhuri ya
Korea, Lee Nak-yon wakati alipoondoka kwenye uwanja wa ndege wa Julius
Nyerere jijini Dar es salaam baada ya ziara ya siku tatu nchini, Julai
23, 2018.
Ndege
iliyombeba Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Korea, Lee Nak - yun ikiruka
kwenye uwanja wa ndege wa Julius Nyerere baada ya kiongozi huyo kumaliza
ziara yake ya siku tatu nchini Julai 23, 2018
Ndege
iliyombeba Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Korea, Lee Nak - yun ikiruka
kwenye uwanja wa ndege wa Julius Nyerere baada ya kiongozi huyo kumaliza
ziara yake ya siku tatu nchini Julai 23, 2018.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri wa
Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola, akizungumza na mdau wa maendeleo mjini
Arusha,Hans Pol.Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha,Mrisho Gambo.Waziri Lugola yupo
mkoani Arusha kwa ziara ya kikazi
Waziri wa
Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (wapili kushoto), akimsikiliza Kamanda wa Polisi Mkoa wa
Arusha, Ramadhani Ng’anzi (kulia) baada ya kutoka kutembelea
Kituo cha Polisi Utalii.Wapili kulia ni
Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo.
Waziri wa
Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola, akimsikiliza mmoja wa wananchi waliofika
Kituo cha Polisi kupata huduma,Waziri Lugola yupo mkoani Arusha kwa ziara ya
kikazi.
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (wapili kushoto), akiongozana na Naibu
Waziri Kazi, Vijana na Ajira, Anthony
Mavunde (kulia) na Mkuu wa Mkoa wa
Arusha, Mrisho Gambo (wapili kulia), kutembelea eneo la Kaloleni zilipo nyumba
za polisi, jijini Arusha.Kushoto ni mmoja wa wadau waliojitolea kujenga nyumba
hizo,Hans Pol.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola, Naibu Waziri Kazi, Vijana na Ajira, Anthony Mavunde (kushoto) na Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo (kulia),wakisikiliza taarifa ya Kituo cha Polisi Utalii baada ya viongozi hao kutembelea kituo hicho.(PICHA NA WMNN)
No comments :
Post a Comment