NA
K-VIS BLOG, Khalfan Said
ALIYEKUWA
Mpiga picha mashuhuri wa mgazeti ya Chama Cha Mpainduzi (CCM) ya Uhuru na
Mzalendo, Mwalimu Omary amefariki dunia mapema leo alfajiri Julai 25, 2018,
akiwa na umri wa miaka 86.
Kwa
mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Julai 25, 2018 na mtoto mkubwa wa marehemu,
Bw. Omary Mwalimu Omary imesema Mwalimu Omary amefariki leo alfajiri Julai 25,
2018 wakati akipatiwa matibabu kwenye Hospitali na
Chuo Kikuu Cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) kampasi ya Mloganzila, nje kidogo ya jiji la Dar es salaam
“Mzee
alianza kulalamika kuumwa tumbo wiki mbili zilizopita na kufuatiwa na kupooza
mkono na mguu, ambapo kabla ya kufikishwa hapa Mloganzila, Mzee tulimpeleka
hospitali za Magomeni Mapipa na kuhamishiwa Mwananyamala kabla ya kuletwa huku
Mloganzila kufanyiwa vipimo vya kichwa.” Alisema.
Bw.
Omary alisema, Mwalimu Omary ambaye alifanya kazi kwa miaka mingi kwenye
magazeti ya Uhuru na Mzalendo, alipata nafuu kidogo na aliweza hata kuzungumza nae.
“Nakumbuka
mara ya mwisho (jana Julai 24, 2018) Mzee aliniambia nimletee fulana yake
iliyoandikwa Uhuru na Mzalendo, na kweli nilikuwa nimemchukulia leo hii,
lakini nilipofika nikakuta kitanda chake kiko tupu, na baada ya kuuliza
nikaambiwa na manesi pole, mzee ametutoka,” Alisema Bw. Omary katika mahojiano kwa njia ya simu.
Aidha
Bw. Omary amesema, mipango ya mazishi inafanywa nyumbani kwa marehemu Mburahati
jijini Dar es Salaam.
Mwalimu
Omary ameacha mke, watoto wanne na wajukuu 11.
Mwenyezimungu
ailaze roho ya marehemu mahala pema peponi AMIN.

No comments :
Post a Comment