Sunday, July 22, 2018

"NINJA" AWAONYA WANAOBEZA MAMLAKA YAKE,NI WAZIRI KANGI LUGOLA


 
NA K-VIS BLOG

WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Kangi Lugola “Ninja” amewaonya wale wanaobeza mamlaka aliyo nayo dhidi ya walio chini ya wizara yake.

Ninja ameyasema hayo wakati akijibu maswali ya waandishi wa habari waliotaka kujua kama hatua yakle ya sasa ya kumuamuru Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP), kuhakikisha mbwa wa polisi aliyekuwa doria pale bandari kuu ya Dar es Salaam ambaye hajulikani aliko apate maelezo yuko wapi.

Na kama hiyo haitoshi, “Ninja” pia aliagiza ifikapo Julai 31, 2018, IGP ahakikishe popote pale alipo mfanyabiashara Lugumi anamfikisha ofisini kwake.
“Wapo waliopita, na kumbuka waliopita hawakuwa Maninja, sasa kaja Ninja anamtaka Lugumi aje na lazima aje sasa akija ni ni kitatokea, nadhani na nyinyi kama sababu ni waandishi bila hata kufundihwa mtataka kujua.” Alisema Mheshimiwa Lugola ambaye aaliwahi kumuomba mwenyekiti wa kikao cha Bunge, Mhe. Mussa Azamn Zungu, amruhusu avae Kininja, ili asione aibu kuwasema viongozi walioytuhumiwa kwenye kashfa ya Escow.

Hata hivyo kufuatia maagizo hayo, Mhe. Lugola amesema, wapo watu wameanza kubeza maagizo yake kupitia mitandao ya kijamii kwa lengo la kumchonganisha yeye na maafisa hao wa vyombo vya ulinzi vilivyo chini ya wizara yake.

“Nimekwisha wafuatilia wawili ninao hapa, sasa ipo siku nitaruka nao hawa.” Alisema.

No comments :

Post a Comment